HATUPO KWA AJILI KUFUNGIA KAZI ZA WASANII BALI TUPO KWA AJILI YA KUKUZA TASNIA YA SANAA KWA MAPANA - BASATA | ZamotoHabari



Na.Khadija Seif Michuzi Tv


BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewakumbusha wasanii kuwa hawana lengo la kufungia kazi ya msanii bali wapo Kwa ajili ya kuzungumza na kurekebisha kazi ili kuikuza tasnia ya Sanaa kwa mapana.

Akizungumza kauli hiyo Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Kedmon Mapana wakati wa kuwapa nasaha na baraka pamoja na kupokea maoni yao Huku akiwakabidhi bendera washiriki wa tuzo za zikomo zilizowajumuisha wasani wa Filamu, wabunifu wa Mavazi,wasanii wa vichekesho, watangazaji,wapiga Muziki ambao wanatajiwa kwenda nchini Zambia kwa ajili ya kilele cha fainali hiyo inayotarajiwa kufanyika rasmi mwezi octoba Jijini Lusaka nchini Zambia.

Mapana amefafanua zaidi kuwa kwa sasa watanzania wawapigie kura nyingi washiriki hao ambao kwa upande wa Tanzania tunagombea tuzo 50 katika vipengele tofauti tofauti.

"Watakaoshiriki wote tutawapatia vyeti vya kutambulika mchango wao katika ushiriki wao na kwa washindi pia watapewa zawadi hivyo tutawaandalia usiku wao wa kuwapongeza Ili waweze kuona basata sio sehemu ya kuwafungia tu kazi zao au kutoa vibali bali pia no sehemu ya kuchagiza na kutoa hamasa pale taifa linapokua nje kwenye vinyang'anyiro vya tuzo za Kimataifa."

Hata hivyo mapana amesisitiza zaidi kuwa wasanii wanatakiwa kujisajiri basata Ili waweze kupata fursa na vipaumbele mbalimbali vinavyotokea ikiwemo kupatiwa mikopo kwa wasani ambao kigezo cha kwanza ni kutambulika kisheria na baraza la sanaa(BASATA).

Kwa upande wake Mbunifu wa Mavazi nchini Martin Kadinda amewaomba basata kuwashika mkono katika safari ya kuelekea zambia Kwa upande wa usafiri ili washiriki waweze kumudu kusafiri ili kupata hamasa zaidi na kurudi na ushindi wao.

"Tungependa tuweze kushirikiana na shirika la ndege kuona kwa kiasi gani tunaweza kupunguziwa gharama za usafiri ili Kwa uchache wetu tuweze kufika mji wa Lusaka nchini Zambia kwenye fainali za tuzo za zikomo."


Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Kedmon Mapana akizungumza na washiriki wa tuzo za zikomo Jijini Dar es salaam,ambapo tuzo hizo zilizowajumuisha wasanii , wabunifu,wapigaji Muziki pamoja na wanahabari nchini huku akiwasisitiza zaidi kuwa basata itaendelea kushirikiana nao ili kuwapa hamasa ya ushindi katika tuzo hizo zinazofanyika jiji la Lusaka nchini Zambia


Miongoni mwa washiriki wa tuzo za zikomo katika vipengele mbalimbali akiwemo mchekeshaji Lucas Mhuvile maarufu "Joti" wakisikiliza mawili matatu kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) akiwapa neno la faraja


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini