MASHINDANO YA MUNGAI MEMORIAL CUP KUTIMUA VUMBI JUMAMOSI | ZamotoHabari

Mashindano ya Mungai Memorial cup yanatarajia kutimua vumbi jumamosi tarehe 31 septemba katika viwanja vya Wenda yenye lengo la kumkumbuka mzee Joseph Mungai pamoja na kudumisha umoja

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya mufindi Mh Saad Mtambule amesema mashindano hayo yanaenda kuongeza ushirikiano kwa vijana pamoja na kujiepusha na vitendo vya ukatili.

Aidha Mtambule amebainisha kuwa kupitia mashindano hayo ya Mungai memorial cup yanaenda kurejesha heshima ya soka katika wilaya ya mufindi iliyofifia kwa miaka ya hivi karibuni

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya mufindi Gift Mwachan'ga amesema wamejipanga vyema kuendesha mashindano hayo yatakayowakutanisha timu mbalimbali pamoja na kuibua vipaji

Miongoni mwa timu zitakazoshiriki mashindano hayo ni misitu fc pamoja na bajaji fc kwa upande wao wamejinasibu kufanya vyema katika mashindano hayo na kutwaa kikombe hicho

Mashindano hayo yatashirikisha takribani timu nane kutoka wilaya ya mufindi huku mtindo utakaotumika ni mtoano mpaka kufikia hatua ya fainali mnamo tarehe 13 ya mwezi wa kumi 2022.









Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini