Picha ya pamoja.
Wachezaji wa Timu za Mchezo wa Kikapu wakicheza Mpira huo katika Viwanja vya Gymkana jijijni Dar es Salaam baada ya kukarabatiwa.
KAMPUNI MMI inayomiliki kinywaji cha Hennessy na NBA wakishirikiana katika kukarabati uwanja wa Kikapu katika viwanja vya wazi vya mchezo wa Kikapu uliopo katika barabara ya Obama jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng'wilabuzu Ludigija akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 10,2022 wakati wa uzinduzi wa viwanja hivyo vya Mchezo wa Kikapu amesema kuwa uwanja huo kabla na baada ya ukarabati unatumika na watu wote.
"Tunawapongeza sana Kampuni ya kinywaji cha Hennessy na NBA kwa kuunga mkono juhudi za serikali, kwa kuinua michezo katika nchi yetu na kukarabatia uwanja huu na lengo la kukarabati uwanja huo ni kuhamasisha wananchi na vijana kucheza mpira wa Kikapu."Amepongeza Ludigija
Amesema kuwa serikali inatambua kuwa Mpira ni ajira na umevuta vijana wengi na hakuna sababu ya kuacha kuunga mkono juhudi za wadau wa mchezo huo katika kuuendeleza.
Amesema baada ya kampuni hiyo kuukarabati lakini wataendelea kuusimamia na kukarabati kwa miaka mitatu.
Ludigija amesema kuwa serikali inampango wa ujenzi wa shule ya michezo mbalimbali ikiwamo mchezo huo wa kikapu.
Ludigija amewaomba kampuni ya MMI waendelee kushirikiana na serikali katika kuendeleza Viwanja vya michezo mbalimbali kwani michezo inatoa ajira kwa Vijana wengi nchini.
Amesema Kwa upande wa Dar es Salaam ujenzi wa shule ya michezo umeshaanza katika eneo la Msongola ambapo watatoa mafunzo ya michezo.
Amesema Vijana watakao kuwa wanahitimu katika shule hizo watakuwa wanafanyia mazoezi katika viwanja vya wazi.
Licha ya hayo Ludigija amewaomba Vijana, wanafunzi na wananchi kwa ujumla wa Ilala kwenda kutumia uwanja wa kimataifa ulio karabatiwa kwaajili ya kucheza mchezo wa Kikapu.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Timu ya Spider Club, Rwagga Lupara amewashukuru kampuni ya MMI yenye kinywaji cha Hennessy kwa kufanya ukarabati katika viwanja hivyo vya wazi na kuboresha mazingira kwani hawakutarajia kuwa patakuja kufanyiwa ukarabati mkubwa.
Pia amewaomba wadau wa michezo wasaidie ujenzi wa Choo na vyumba vya kubadilishia nguo wakati wanamchezo huwa wakiwa katika viwanja hivyo wakicheza na kufanya mazoezi.
Meneja Masoko wa nchi za Afrika Masharika na Afrika ya kati wa Moet Hennessy, Janet Mwalilino amesema kuwa kwa Nchi za Afrika uwanja wa Mpira wa Kikapu wa Gymkana ni wa kwanza kukarabati kwa kiwango cha kimataifa. Amesema uwanja huo ni moja kati ya viwanja vinne ambavyo Kampuni ya MMI kuwahi kukarabati Barani Afrika.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments