Na.Khadija Seif, Michuzi Tv
MKUU wa Mkoa wa Mtwara amefungua rasmi zoezi la ununuzi wa tiketi za pambano la kitaifa kati ya Bondia Twaha Kiduku na mpinzani wake kutoka Misri linalotarajiwa kufanyika septemba 24 mwaka huu katika uwanja wa Nangwanda sijaona Mkoani Mtwara.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa zoezi hilo Kanali Ahmed abbas amesema ni wakati wa Wakazi wa Mtwara na vitongaji vyake kushuhudia burudani ya Mchezo wa Masumbwi Huku akiwahimiza wafanyabiashara kutumia pambano hilo kama fursa ya kibiashara.
"Wananchi washiriki katika ununuzi wa tiketi ili waweze kushuhudia mpambano huo ambao mtanzania mwenzetu anaenda kuliwakilisha Taifa Kimataifa."
Hata hivyo amemsihi Bondia Twaha Kiduku ajitahidi kufanya vizuri kwani Taifa limemuamini na limempa dhamana hivyo afanye vizuri ili asiwaangushe watanzania na Mashabiki wa Masumbwi.
Pia ameongeza kuwa mbali na pambano hilo litaambatana na shamra shamra za kutembelea vivutio vya utalii katika mji wa kihistoria wa Mikindani septemba 27 mwaka huu mara baada ya kuisha kwa pambano hilo la "Ubabe ubabe 2".
Kwa upande wake Naibu Mstahiki Meya Manispaa ya Mikindani Edward Kapwapwa ametoa pongezi nyingi kwa waandaaji wa pambano hilo Kampuni ya Peaktime Media kwa kuchagua Mkoa wa Mtwara kupata ugeni huo mkubwa wa Kimataifa.
"Tunashahuku kubwa kuona pambano hili linafanyika na tumejiandaa vya kutosha katika kuona mji wetu unakua na Mtwara inafunguka na kwa mara ya kwanza hili jambo limekua jipya na la kushtua kutokana na Mikoa ipo mingi lakini Mkoa wetu umepata bahati ya kipekee ya kupokea ugeni mzito kwa pambano la Kimataifa.
Aidha,Meya ametoa wito kwa wakazi wa Mtwara na Mikoa ya jirani ikiwemo Lindi,Tunduru na Songea kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Nangwanda sijaona pamoja na kujumuika.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas akiwa na tiketi za pambano la kitaifa la "ubabe ubabe 2" mara baada ya kufungua rasmi zoezi hilo la ununuzi wa tiketi ambapo pambano hilo litamkutanisha Bondia Twaha Kiduku dhidi ya mpinzani wake Abdo Khaled kutoka Misri katika viwanja vya Nangwanda sijaona Mkoani Mtwara septemba 24 mwaka huu
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments