MWAKINYO 'AKAMIA' KUMSHUSHIA KICHAPO SMITH | ZamotoHabari


*Awaomba watanzania kufanya Dua kwa ajili yake

Na Khadija Seif, Michuzi Tv
BONDIA namba moja nchini katika ngumi za kulipwa, Hassan Mwakinyo ameondoka tayari kwa pambano lake dhidi ya Liam Smith wa Uingereza huku akiahidi kumchapa mpinzani wake katika pambano litakalopigwa septemba 03 mwaka huu.

Mwakinyo atapanda ulingoni kwenye pambano hilo la raundi 12 katika uzani wa Super Walter pambalo litapigwa kwenye Ukumbi wa M & S Bank Arena uliopo katika Jiji la Liverpool nchini Uingereza.

Mwakinyo amesema kuwa anapata faraja kubwa kutoka na watu walionyuma yake kubeba matumaini makubwa kutokana na imani ambayo ameitengeneza kwao huku akisisitiza atahakikisha mpinzani wake anamueleza kwa nini mama yake alikufa kirahisi.

"Nataka niwaambie kwamba nina pambano Septemba 3, mwaka huu dhidi ya Liam Smith wa Uingereza ambaye ni bondia namba sita kiubora duniani, namba moja Jumuiya ya Madola lakini mimi ni namba moja Tanzania na Afrika na 34 kidunia na nimeshuka viwango kwa sababu ya muda mrefu kutopigana kutokana na msiba wa mama yangu.

"Nimekamia kweli, naamini atanieleza kwa nini mama yangu alikufa kirahisi kwa sababu naamini nilikuwa na sababu ya kumfanya aendelee kuishi japokuwa mauti ni siri ya Mungu, hii inaonyesha ni kiasi gani nitakwenda kumuumiza na sihofii chochote, ninachohitaji ni dua na maombi yenu."


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini