TUMIENI MICHEZO KUJENGA MAHUSIANO MAZURI YA KIBIASHARA NA MAHALI PA KAZI | ZamotoHabari



Na.Vero Ignatus,Arusha

Mechi ya kirafiki baina ya Mervec hotel na Taasisi ya Sibusiso inayowalelea watoto wenye mahitaji maalum umefanyika katika viwanja vya sibosiso wilayani Arumeru mkoani Arusha ,imemalizika huku timu ya sibosiso kuibuka mshindi wa magoli 2 huku timu ya Marves ikiambulia goli 1

Akizungumza Meneja wa Marvec hotel Mathew Peter Kabaa amesema timu hiyo ilianzishwa kwa lengo la kuhamasisha sensa ya watu na makazi vilevile kwaajili ya kuimarisha Afya kwani baadhi ya wageni wanaokuja kupumzika hotelini hapo waweze kufanya mazoezi kwaajili ya Afya zao


Kabaa amesema hoteli hiyo ya Marves imekuwa ikipokea wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kwahiyo majira ya jioni wamekuwa wakishiriki mazoezi kwaajili ya kujenga Afya zao. 


Akizungumza kocha wa timu ya Marves Eric Hendry Msaki mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, alisema kuwa mchezo ulikuwa mzuri huku akitunisha misuli kwamba katika mechi ya marudiano nitakayofanyika wiki ijayo viwanjani hapo wataibuka na ushindi

"Timu yangu bado changa na imeshindwa kufanya vizuri kwasababu ya maandalizi, na hatukua na mazoezi,kwani tumefanya zoezi kwa siku tatu tu, vip kama tungelikuwa tumefanya zoezi kwa mwezi mzima ingekuwa shughuli ,nafikiri tuanamechi ya marudiano siku ya ijumaa tutawaonyesha kwamba Merves ninini"alisisitiza Msaki

Kwa upande wake kocha wa timu ya Sibosiso Stanford Chalamaganza amesema vijana walijinoa kwa wiki tatu kwaajili ya mechi hiyo, na wapo kwenye mazoezi magumu na ndiyo maana wameweza kuibuka kidedea kwa kuwatandika bao mbili

Kwa upande wake Kapteni wa timu ya Marves Ditric Dismas amesema kuwa timu yake ilishindwa kufanya vizuri mbele ya sibosisu kwasababu wachezaji hawakuwa na maandalizi ya mazoezi


" Ni kweli leo wamevamia mtumbwi wa vibwengo hatujafanya vizuri ila tunaahidi gemu inayokuja tutafanya vizuri kabisa na tutawaoiga zaidi ya goli tano " Alisema Kapteni wa timu hiyo

Naye Mratibu wa bonanza hilo Terry Mushi amesema kuwa limejenga kujenga Afya na mahusinao kati yao na kibiashara kati ya Kituo hicho cha watu wenye ulemavu cha sibosiso na hotel ya Marves ambapo wataendelea na mabonaza mbalimbali ikiwa ni kuboresha Afya mahala pa kazi


"Bonanza hili Kwaajii ya kujenga urafiki na undugu kwasababu sisi tunafanya semina katika kituo chetu,na wanasemina wanalala katika hotel ya Marves hivyo ili kuonyesha tupo pamoja na wao ndoyo maana tumeona tiwe pamoja na ushirikiano wa karibu zaidi kama michezo ili kuonyesha michezo na umoja".


Mechi hiyo imemalizika huku Sibosiso wakijipatia magoli mawili na Marves wakipata bao moja ambapo mechi hiyo ililalamikiwa kutokana na muamuzi kutoeleweka.

Timu ya Marves Hotel wakiwa katika picha ya pamoja katika uwanja wa kituo kinachoshughulika na watoto wenye ulemavu cha Taasisi ya Sibusiso Iliyopo mkoani Arusha
Kocha wa Marves Erick Hendry Msaki akizungumzia juu ya namna ambavyo wmaejipanga kwa mechi ya maridiano ijumaa ijayo ambapo amehigamba kwamba lazima waibuke kidedea kwa kuwafunga wapinzani wao goli 5
kocha wa Timu ya Sibosiso Stanford Chalamaganzaakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mechi hiyo kumalizika

Kapteni wa timu ya Marves Ditric Dismas:Wapinzani wetu wamevamia mtumbwi wa vibwengo,hapa wajiandae kwa mechi ya marudiano Ijumaa ndipo watatuelewa vyema kwamba hatuna mchezo ni mwendo wa kuwacharaza mabao tu
Kapteni wa timu ya sibosiso Israel John Shevadizo,sisi ushindi wetu siri kubwa ni mazoezi,tunawaahidi mechi ya marudiano ijumaa wajiandae magoli ya kutosha.




Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini