Kikosi cha KMC FC kesho kitashuka katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania bara dhidi ya Azam utakaochezwa saa 16:00.jioni.
KMC FC chini ya kocha mkuu Thierry Hitimana imefanya maandalizi ya mwisho na yamekamilika kwa asilimia kubwa na kwamba wachezaji wote wapo tayari kwa mtanange huo.
Katika mchezo huo Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni itakuwa nyumbani na kwamba wachezaji wamejiandaa kuhakikisha kuwa licha ya kuwa na ushindani wa Ligi lakini watahakikisha kuwa alama tatu muhimu zinabakia nyumbani.
"Tunakwenda kwenye mchezo wenye ushindani mkubwa , ambao tunahitaji ushindi, Azam ni Timu nzuri , wanawachezaji wazuri hivyo tunawaheshimu lakini KMC ni bora zaidi na kwamba kila mchezaji amejiandaa kutumika vizuri ili kupata alama tatu.
Tunajivunia kuwa na wachezaji wenye ubora na ambao siku zote wamekuwa wakijitoa kwa ajili ya Manispaa ya Kinondoni, kila mmoja anafahamu umuhimu wa mchezo huo , hivyo wana Kinondoni wote, mashabiki zetu kutoka maeneo mbalimbali mjitokeze kwa wingi kuwasapoti wachezaji wetu.
Kwa upande wa Afya za wachezaji wote wanahari nzuri, morali na nguvu ya kutumika kwa ufanisi mkubwa, hivyo mashabiki wasiwe na hofu Benchi la Ufundi limefanya kazi kubwa ya kuwaanda wachezaji kwa mafanikio makubwa yakuleta matokeo chanya.
Hata hivyo KMC FC katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC ipo katika nafasi ya sita ,ikiwa imecheza jumla ya michezo saba na kushinda miwili , kutoa sare michezo minne huku ikipoteza mchezo mmoja na hivyo kujikusanyia jumla ya alama 10.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments