KMC FC KUWAKARIBISHA MTIBWA SUGAR KESHO UWANJA WA UHURU | ZamotoHabari


Kikosi cha KMC FC kesho kitashuka katika Dimba la Uhuru Jijini Dar es Salaam kuwakaribisha Mtibwa Sugar ya Manungu Mkoani Morogoro kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara utakaochezwa saa 16:00 jioni.

Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni, inayonolewa na Kocha Mkuu Thierry Hitimana imefanya maandalizi ya mwisho na kwamba ipo tayari kwa mtanange huo ambao kimsingi utakuwa naushindani mkubwa.

Katika mchezo huo KMC FC itakuwa nyumbani kwa mara nyingine tena ambao pamoja na ushindani uliopo imejiandaa kuhakikisha kwamba kama Timu inapata ushindi muhimu hapo kesho.

" Tunakwenda kwenye mchezo mwingine tukiwa nyumbani, tunawaheshimu wapinzani wetu Mtibwa Sugar kwa kuwa ni Timu nzuri na wao pia wanahitaji matokeo, lakini pamoja na hayo kama Manispaa ya Kinondoni tumejipanga kupata ushindi licha ya kwamba katika mchezo uliopita tulipata sare hapa nyumbani.

Tuna amini kuwa matokeo mazuri tutayapata kutokana na kwamba KMC FC tunawachezaji wazuri na wenye ubora mkubwa ambao wanaweza kupambana kutafuta matokeo, na siku zote Timu Bora huwa haitoki sare mara mbili kwenye uwanja wa nyumbani.

Kwa upande wa Afya za wachezaji wote wako vizuri isipokuwa Ibrahimu Ame, Emmanuel Mvuyekure pamoja na Kelvin Kijili ambao wanachangamoto ya majeraha waliyoyapata wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni uliochezwa siku ya Jumanne ya Oktoba 11 na kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Hata hivyo mbali na wachezaji hao kuwa na changamoto ya majeraha, lakini wachezaji wengine wana hari na morali nzuri , kikubwa mashabiki, wana Kinondoni kesho wajitokeze kwa wingi kutoa sapoti kwa vijana wetu ambao wanaenda kupambania alama tatu muhimu.


 


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini