LUGARAWA YOUTH FOUNDATION KUWAKOMBOA VIJANA. | ZamotoHabari


Na. Damian Kunambi, Njombe

Imeelezwa kuwa wazazi kutowajibika katika malezi ya watoto wao na kuwaacha wakijilea wenyewe ni miongoni mwa sababu zinazopelekea kuwepo kwa mmong'onyoko wa maadili kwa vijana na kujihusisha na makundi mbalimbali ya kiuahalifu.

Hayo ameyasema mkurugenzi wa taasisi ya LUGARAWA YOUTH FOUNDATION Romanus Mgimba wakati wa uzinduzi wa taasisi hiyo uliofanyika katika kata ya Lugarawa wilayani Ludewa mkoani Njombe ikiwa na kaulimbiu ya vijana tujitambue tuwe wazalendo, tuwawezeshe vijana kiuchumi, tujikinge na magonjwa yasiyo ambukiza, tuwe tayari kupima virusi vya ukimwi, tupate chanjo ya uviko 19 na tuache kujiingiza kwenye madawa ya kulevya.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa vijana wengi wa sasa wamekuwa wakiunda makundi mabaya kama panya road na kuleta madhara kwa jamii hivyo taasisi hiyo itasaidia kuwaelimisha vijana na kuwafanya wazitambue fursa zilizopo katika maeneo yao.

Akizindua taasisi hiyo meneja wa Tume ya kikristo ya huduma za jamii (CSSC) kanda ya kusini Sylvester Mdope amepongeza hatua hiyo iliyofikiwa na kuongeza kuwa vijana wanapowekwa pamoja na kupewa maarifa itasaidia kuwafanya waweze kuwajibika katika shughuli za kiuchumi na kuinua Taifa.

Amesema serikali pamoja na taasisi mbalimbali zinapaswa kuwaangalia vijana kwa jicho la kipee ili kuokoa vizazi vya sasa na baadae.

Patrick Nombo ni mjumbe wa bodi wa taasisi ya LUGARAWA YOUTH FOUNDATION na mratibu wa michezo mbalimbali amesema ili kuwakusanya vijana pamoja wameweka michezo mbalimbali pamoja na kutoa huduma ya afya hasa kwa magonjwa yasiyo ambukiza kwakuwa magonjwa hayo yamekuwa yakisaulika katika kupatiwa matibabu.

Pia amesema miongoni mwa michezo iliyofanyika ni kukimbiza kuku, kukimbia na magunia, kuvuta kamba pamoja na ligi ya mpira wa miguu iliyohusisha timu 8 za kata ya Lugarawa inayotarajiwa kuhitimishwa October 30 mwaka huu huku bingwa wa ligi hiyo atajinyakulia kitita cha sh. Laki 5, mshindi wa pili laki 3 na mshindi wa tatu laki 2.








 


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini