Na Mwandishi wetu
Kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-Bet Tanzania imeipongeza klabu ya Simba kwa kuwa timu pekee Tanzania kuingia hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika kwa mara ya nne katika historia.
Agosti Mosi mwaka huu, M-Bet Tanzania ilisaini mkataba wa miaka mitano na Simba wenye thamani ya Sh26.1 bilioni na kuwa timu ya kwanza kuingia mkataba mnono zaidi wa udhamini nchini.
Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema jana kuwa wanajivunia mafanikio ya Simba ikiwa wanaelekea katikati ya msimu tangu kampuni yao kuingia udhamini wa miaka mitano na klabu hiyo.
Mushi alisema kuwa M-BET inajisia faraja kubwa kuona timu inayoidhamini kufanya vizuri katika ligi ya Mabingwa Afrika na hata ligi ya ngumbani ambapo kwa sasa inaongoza ligi.
“M-Bet ndiyo wadhamini wakuu wa klabu ya Simba na matunda ya udhamini wetu yameanza kuonekana kwani Simba itaendelea kulinda chapa yao huku ikiitangaza nchi nje ya mipaka yake kupitia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Lengo la M-Bet ni kuchangia mafanikio ya Simba na mpira wa Tanzania na mpaka sasa matunda yameanza kuonekana kwani ni wazi kuwa wanachama, mashabiki na wadau wengine wa mpira wa miguu wanafurahia mafanikio ya klabu hiyo mpaka sasa,” alisema Mushi.
Alisema kuwa Simba imekuwa ikifanya vyema katika mashindano ya kimataifa kwa miaka mingi, lakini mwaka wa kukumbukwa sana ni 2003 ambapo timu hiyo ilifuzu hatua ya makundi kwa kuitoa timu ya Zamalek ya Misri kwenye uwanja wao wa nyumbani.
“Simba pia ilifikia hatua ya makundi mwaka 2018/2019, 2020/2021 na msimu wa mwaka huu ambapo droo yake itafanyika mwezi ujao. Tunawaomba mashabiki kuendelea kuipa sapoti Simba katika hatua inayofuata na vile vile kubashiri na M-Bet kwani ni ‘simpo’ tu,” alisema.
Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi akisisitiza jambo wakati wa kutangaza salamu maalum za pongezi kwa klabu ya Simba kwa kuwa timu pekee iliyoweza kufuzu hatua ya makundi katika ligi ya mabingwa afrika kwa mara ya nne katika historia.
Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya M-BET Tanzania, Allen Mushi akizungumza wakati wa uzinduzi wa udhamini wa miaka mitano na klabu ya Simba ambapo kampuni hiyo imetenga Sh bilioni 26.1 kuidhamini Simba
Wachezaji wa Simba wakiwa katika picha ya pamoja
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments