MSIMU WA PILI WA TAMASHA LA TUZO ZA FILAMU WAFUNGULIWA | ZamotoHabari


Na.Khadija Seif, Michuzi Tv 


MSIMU wa pili wa Tuzo za Filamu nchini zimezinduliwa rasmi huku Bodi ya Filamu ambao ndio waandaaji wakuu wa tuzo hizo wakiaHidi maboresho mbalimbali kunogesha usiku huo Mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi wa wahabari,wasanii na wadau wa Filamu nchini septemba 30 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Kiagho Kilonzo amesema ni Msimu wa pili wa tuzo za Filamu nchini ambapo maboresho yamefanyika Ili kuleta utofauti katika Tamasha hilo.

"Maboresho hayo ni pamoja na namna ya uwasilishaji wa kazi za wasanii ambapo Kuna baadhi ya mikoa itapata nafasi ya kupokelewa kazi zao ikiwemo Dar es salaam,Mwanza,Tanga , Morogoro pamoja na Mbeya ."

Hata hivyo Kilonzo ameongeza kuwa kwa Msimu huu wa pili vipengele 31 vitashindaniwa vya tuzo za Filamu.

"Ikiwemo Msanii Bora wakike na wakiume,Tuzo ya heshima kwa Msanii wakike na upande wakiume, Mchekeshaji bora wa Mitandaoni pamoja na vipengele vingine."

Aidha Vigezo vya kushiriki tuzo hizo zinahusisha watayarishaji wa Filamu za lugha ya kiswahili kutoka Tanzania pekee, ambapo Filamu zitakazoshindanishwa ni zilizoandaliwa kuanzia januari hadi julai mwaka huu.

Pia Kilonzo ameomba wadau na taasisi mbalimbali wajitokeze kudhamini Tamasha hilo Huku akisisitiza kuwa wadhamini watakaojitokeza hakutakua na muingiliano wa kibiashara katika kujitangaza kwao watazingatiwa ipasavyo kuhakikisha wananufaika kupitia Tamasha hilo na kuwakumbusha wadau na wasanii kuwa rasmi septemba 30 wameanza kupokea kazi zitakazoshindania tuzo hizo huku zoezi la upigaji kura kuwapa fursa wenye simu za vitochi pia.

Kwa upande wa Msanii bora wavichekesho Lucas Mhuvile maarufu kama Joti amesema kurudi kwa Msimu wa pili wa tuzo hizo utaleta fursa na chachu kwa Wasanii kuendelea kufanya kazi nzuri zenye ushindani.

"Msimu wa pili wa tuzo za filamu nchini kutapanua soko la filamu na kukuwa Kwa tasnia yetu kutokana na wasanii watatengeneza kazi zenye ubora na shindani".



Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Kiagho Kilonzo akizungumza na wadau wa Filamu mara baada ya kutangaza rasmi uzinduzi wa Msimu wa pili wa tuzo za Filamu uliofanyika katika ukumbi wa Sheraton Hotel jijini Dar Huku kauli mbiu ya Tamasha hilo ikiwa "Filamu ni Biashara" ambapo lifanyika jijini Arusha


 Mkongwe wa tasnia ya Filamu Mzee Hashim Kambi,Katty pamoja Mwenyekiti wa wasanii Chiki Mchoma pamoja na Mtayarishaji wa Filamu Abdul Usangi wakisikiliza kwa makini taarifa ya uzinduzi wa Msimu wa pili wa tuzo za Filamu nchini kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Kiagho Kilonzo alipokua anazungumza katika ukumbi wa Sheraton jijini Dar es salaam



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini