RAIS SAMIA MGENI RASMI KATIKA MJADALA WA KITAIFA WA NISHATI UTAKAOFANYIKA NOVEMBA 1-2, 2022 DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika mjadala wa kitaifa wa utaokuja na suluhu ya namna watanzania watakavyohamasika na matumizi ya Nishati mbadala na kuachana na nishati isiyofaa. 

Mkutano huo utakaofanyika Novemba 1-2, 2022  katika Kituo cha cha Kimataifa cha Mikutano cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam utaratibiwa na Wizara ya Nishati.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Oktoba 12, 2022. Waziri wa Nishati Januari Makamba amesema kuwa mkutano huo utawakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta za Afya, Nishati, Mazingira, Jinsia, Usawa watunga sera pamoja na sheria mbalimbali ili kuweza kujadiliana namna gani wanaweza kupunguza au kuondoa kabisa matumizi ya nishati ya isiyo safi na salama. 

Amesema Sera ya Nishati ya 2015 inayosimamiwa na wizara ya nishati inaelekeza Wizara ya Nishati kuchukua hatua za kuwawezesha watanzania kupata nishati safi na salama na kwa gharama wanayoimudu ili kuboresha ustawi wa watanzania kwa kiasi kikubwa. 

Waziri makamba amesema kuwa Mjadala huo utaratibiwa na wizara ya Nishati ili kupata majibu ya kudumu ya kuondokana na matumizi ya nishati ya kupikia ya Mkaa na kuni nchini pamoja na kupata uelewa wa pamoja juu ya suala nishati ya kupika hapa nchini.

Amesema kuwa katika mkutano huo watangazi katika mlengo wa kiuchumi, Kijinsia afya Usawa na mazingira kwa namna ambavyo tunapika hapa nchini kwa kutumia Nishati safi na Salama. 

Waziri Makamba amesema mjadala huo utapelekea kutambua Changamoto za kutumia kuni na Mkaa, athari zilizipo na kuangalia matokeo yake ni nini. 

Amesema Mifumo ya Kisera Sheria, Kikodi, Kifedha na Utawala itawekwa kwaajili ya kupambana na hali ya namna tunavyopika na kuwaondoa watanzania kutumia nishati inaathiri Afya na Maisha. 

Akizungunzia kuhusiana na madhara yanayojitokeza katika jamii juu ya matumizi ya kuni, Mkaa na nishati nyingine zisizo safi na salama Waziri Makamba amesema Vituo vya afya Nchini vimeelemewa na mzigo Mkubwa wa utoaji huduma za afya za mfumo wa upumuaji zinazotokana na namna tunavyopika.

Amesema Watanzania zaidi ya elfu 33 wanafariki dunia kwa mwaka kutokana na kuvuta moshi wa namna tunavyopika chakula hivyo hii inaendelea kuathiri akina mama na watoto wa kike kwa  kupoteza muda mwingi kwenye kutafuta nishati ya kupikia ya kuni na Mkaa. 

Asilimia 70 ni magonjwa yasiyoambukiza ikiwemwo magonjwa ya mfumo wa upumuaji.

"Wanapokuwa wanatafuta nishati hiyo wanapunguza muda wa kutafuta elimu au kufanya shughuli nyingine za uzalishaji mali huko polini wanakutana na dhahama na matukio ya unyanyasaji wa kijisia.

Pia Nishati  isiyo safi na salama inaleta utofauti au kutokuwa na usawa kati ya wanawake na wanaume, watu wa mjini na vijijini wenye kipato na wasio na kipato." Amesema  Waziri Makamba

Kwa Upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya mfumo wa Upumuaji, kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Pauline Chale ameeleza kuwa Matumizi ya Nishati isiyo safi na salama  inasababisha changamoto nyingi hasa katika Afya na matibabu yake ni gharama kubwa 

Dkt. Pauline ameeleza kuwa mgonjwa wa Mfumo wa Upumuaji yanaondoa watu. Pia amesema matumi ya kuni, Mkaa na Mavi ya wanyama yanasumu zaidi ya 200 ndio maana watu wengi wanakuwa na macho mekundu kutokana na sumu hizinazopatikana kwenye moshi.

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini