SHINDANO VIZIWI TANZANIA ITANYAKUA MATAJI- WAKUFUNZI | ZamotoHabari










Adeladius Makwega-WUSM


Wakufunzi wanafundisha miondoko kwa washiriki wa Tanzania katika kambi inayojiandaa na Mashindano ya Urembo, Utanashati na Mitindo ya Dunia yatakayofanyika Oktoba 29, 2022 jijini Dar es Salaam wamesema kuwa kwa sasa washiriki wote wako vizuri wana ari ya kushiriki na kushinda mashindano hayo.

Haya yamesemwa kwa pamoja na wakufunzi Nasra Swalehe na John Mushi katika kambi hiyo iliyopo Hoteli ya Peacock Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

“Maandalizi ni mazuri, washiriki wanaendelea vizuri, mpaka sasa Watanzania na vijana wenzetu wako na ari ya ushindi, wanajitoa kwa moyo wote kupambania wito wao, kuliwakilisha vema taifa letu.”

Jambo hili limetutia moyo mkubwa na tunahimiza pia kila vijana wa taifa letu wanapopata nafasi ya kutuwakilisha popote pale wajitoa kwa moyo wote na ushindi wao ni wa kila Mtanzania. Vijana wajitokeze kwa wingi kila mashindano kama haya yanapotangazwa,kwani sasa ulemavu siyo kikwazo alisema mkufunzi Nasra Swalehe ambaye aliwahi kuwa Mshindi wa Miss Dar es Salaam mwaka 2021/2022.

Kwa upande wake mkufunzi wa miondoko John Mushi ametoa ahadi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mheshimiwa Samia Sukuhu Hassan na kwa Watanzania wote kuwa ushindi Oktoba 29 ni wetu kwa kuwa viwango vya washiriki vipo juu.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini