Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
TBC wameamua! Ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kutangaza kwamba litakuwa mbashara kwa kuonesha mechi 92 za Kombe la Dunia nchini Qatar zitakazoanza rasmi kuanzia Novemba 20 hadi Desemba 18 mwaka huu.
Uamuzi huo unakuja zikiwa zimebakia siku 30 kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia hivyo mashabiki wa soka nchini watapata fursa ya kushuhudia mitanange hiyo kupitia TBC One,TBC Radio,TBC Taifa na TBC On line.
Akizungumza leo Oktoba 21,2022 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa TBC Dk.Ayub Rioba ameeeleza kwamba katika michuano hiyo ya Kombe la Dunia jumla ya mechi 28 zitatangazwa kupitia TBC One na TBC online na mechi 64 zitatngazwa kupitia TBC Radio yenye kauli mbiu yake ‘MBUNGI NYUMBANI BUUURE’.
“Hili si jambo geni kwetu TBC tuna uzoefu mkubwa wa kurusha Kombe la Dunia historia inaonesha TBC ilishatangaza mashindano haya mwaka 2010, 2014 na fainali za mwaka 2018," amesema Dk. Rioba
Aidha amesema katika fainali hizo za mwaka huu TBC imefanya juhudi kubwa kuhakikisha watanzania wanapata haki ya kuburudika na michuano hiyo mikubwa duniani ambayo hufanyika kila baada ya miaka minne.
Amesema tayari shirika hilo limeanza kurusha vipindi vya matangazo mbalimbali kuhamasisha wasikilizaji na watazamaji wao kuwa tayari kwa michuano hiyo.
Ameongeza kuwa wana kipindi cha GOZI QATAR kinachoruka kwenye Televisheni yao ya TBC One na KIOTA kinachoruka kwenye Radio za mbili za TBC Taifa, TBC Fm na TBC Online ambavyo vyote vinazungumzia na kuhamasisha michuano ya Kombe la Dunia.
Dk. Rioba amefafanua wanavipengere viwili ambavyo vinaruka kwenye vipindi mbalimbali vya Radio na Televisheni ambavyo vinaitwa Nahodha na Chama langu vinavyozungumzia wachezaji na timu mbalimbali zitakazoshiriki fainali za kombe la Dunia Quatar 2022.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments