Na Khadija Seif,Michuzi TV
KLABU ya Rotary yakabidhi madawati 200 kwa Shule ya Msingi Minanzini huku wadau wengine wakiombwa kuboresha miundombinu mbalimbali kwenye shule hiyo ashuleni ili kuwajengea uwezo wanafunzi kufanya vizuri masomo yao.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam Saad Mtambule wakati wa kupokea madawati hayo amesema Rais Dkt.Samia Suluhu ameendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji na wadau kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kusaidia na kutoa michango kwa jamii.
"Wadau wetu wa Rotary Club Dar wametupatia .adawati 200 yenye thamani Sh.milioni 30 pamoja na vitabu kwa Shule ya Msingi Minanzini lakini wadau hawa wamekuwa wakiendelea na utaratibu wa kufika shule mbalimbali.
"Mara ya mwisho walitembelea Shule ya Msingi Mwananyamala B na kugawa Madawati 100 yenye thamani ya Sh. Milioni 13.5. Madawati niliyopokea leo hii yataenda kuleta tija pamoja na kuleta chachu ya maendeleo ya kufanya vizuri kwa wanafunzi hawa."
Pia ametoa rai kwa walimu na wazazi kuhakikisha wanafuata taratibu na sheria ili kutoa adhabu zitakazowaimarisha na kuwajenga wanafunzi kuliko kutoa adhabu zitakazowaumiza na kuharibu saikolojia yao.
Kwa upande wake Rais wa Klabu ya Rotary Nikita Aggarwal amesema wataendelea kugawa madawati kwa shule zenye uhitaji zaidi kadri fedha zinavopatikana kutoka kwenye michango ya wanachama wa Klabu hiyo na marafiki wa Rotary ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira rafiki kwa kusomea.
"Madawati tuliyotoa hadi sasa yamewanyanyua chini watoto zaidi ya 6,000 ambao walikuwa wanakaa chini wakiwa madarasani.Tutaendelea na mradi wa kutoa madawati utakaoenda sambamba na upandaji wa miti ili kuhifadhi mazingira. Hivi sasa mradi wetu huu umeshatoa zaidi ya madawati 2,000 yenye thamani ya Sh.Milioni 300 kwa shule mbalimbali.
Wakati huo huo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Minanzini amewapongeza Klabu hiyo na kuwaomba wasaidie shule zingine ili kuboresha miundombinu mbalimbali na kuweka Mazingira rafiki kwa wanafunzi shuleni.
Mkuu wa wilaya Saad Mtambule akiwa pamoja na Rais wa Klabu ya Rotary Dar wakiendelea na zoezi la upandaji wa miti katika shule ya msingi Minazani iliyopo Kata ya Mwananyamala B Jijini Dar es salaam mara baada ya kupokea msaada wa Madawati 200 yenye thamani ya Shilingi Milioni 30 ikiwa ni sehemu ya zoezi la uchangiaji wa Madawati mashuleni.
Rais wa Klabu ya Rotary Dar es salaam Nikita Arragawal akimpa mkono Mkuu wa wilaya Saad Mtambule pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Minanzini kama ishara ya kukamilika kwa zoezi la ugawaji wa Madawati pamoja na zoezi la upandaji miti.jpeg)

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

0 Comments