Na Shamimu Nyaki
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Pindi Chana amelipongeza Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kwa ujenzi wa Kituo cha Michezo katika Manispaa ya Kigamboni Dar es Salaam ambacho kitasaidia kukuza mchezo wa Soka.
Mhe. Chana ametoa pongezi hizo Februari 20, 2023 wakati alipofanya ziara katika Kituo hicho ambapo amesema Kituo hicho kitasaidia kuzalisha wachezaji makocha na wataalam wa michezo.
"Sisi Serikali tutaendelea kushirikiana na nyie wadau wetu katika kuendeleza michezo ambayo kwa kiasi kikubwa inatoa ajira kwa vijana wetu na kuitangaza nchi kama zilivyofanya Serengeti Girls na Tembo Worrios," amesema Mhe. Chana.
Awali alipozungumza na uongozi wa Wilaya ya Kigamboni, Mhe. Chana ameisisitiza Wilaya hiyo kutenga eneo kwa ajili ya kujenga uwanja wa michezo na kusisitiza Maafisa Michezo kusimamia vyema sekta hiyo katika maeneo yao.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Pauline Gekul amesisitiza Halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya shughuli za michezo ikiwemo ujenzi na ukarabati wa maeneo hayo.
Naye Rais wa Shirikisho hilo, Bw. Wallace Karia ameishukuru Serikali kwa ushirikiano inaotoa katika kuendesha shirikisho hilo ikiwemo kusaidia timu za Taifa katika mashindano mbalimbali.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

.jpg)


0 Comments