CHONGOLO AITAKIA KILA LA KHERI YANGA FAINALI CAFCC | ZamotoHabari

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameitakia kila la kheri Klabu ya Yanga katika mchezo wake wa kwanza wa Fainali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger ambao utachezwa jioni ya leo Mei 28,2023 katika dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Chongolo ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wananchi kwenye kata ya Malangali,Mafinga mkoani Iringa kwenye mkutano wake ambapo pia  amesekuwa Yanga uwezo  wa kushinda wanao na kuweza kuliwakilisha vyema Taifa kwa ujumla.

"Sina mashaka na nafasi walionayo Yanga kuitendea haki kwenye mechi ya leo ili kwenye marudio kule ugenini kazi iwe rahisi,  nategemea ushindi wa kishindo na ndo jambo ambalo litatupa faraja kuhitimisha ziara kwenye jimbo hili". Amesema




Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini