MLELA ATIMKIA KWENYE MASUMBWI ATAMANI KUZICHAPA NA MANDONGA | ZamotoHabari

*Amkanya Mkali wenu kuacha kick boxing Ulingoni *

    Na.Khadija Seif,Michuzi blog 


BAADA ya kupigwa na msanii wa vichekesho, Miraji Fundikila ‘Mkali Wenu’, nyota wa filamu nchini, Yusuph Mlela amesema yupo tayari kurudiana nae pambano hilo.


Mei 5 mwaka huu,  Mlela alipoteza pambano lake mara baada ya kuchakazwa na Mkali Wenu kwa pointi katika mchezo wa ngumi na mateke (kick boxing) lenye uzito wa juu raundi nane.


Akizungumza na Michuziblog Mlela amesema anahitaji kurudiana na Mkali Wenu katika pambano hilo la mchezo wa masumbwi  na si kick boxing.


“Mkali Wenu aliweza kunipiga kwa sababu mimi sijawahi kucheza kick boxing, ila sasa hivi nahitaji kupigana naye katika ndondi  ya kwa lengo la kumfundisha na kumuonyesha uwezo wangu."


Bondia huyo amefafanua kuwa sasa hivi ameingia rasmi katika mchezo huo, hivyo pambano atakalocheza matokeo yatawekwa katika rekodi za boxrec.


 “Baada ya kumaliza pambano langu na Mkali Wenu nahitaji kupigana na bondia, Karim  Mandonga na mabondia wengine ambao wapo katika uzito wangu kilogramu 76 hadi 80.''


Promota wa pambano hilo, Abdul Salimini ambaye pia ni Mkurugenzi wa klabu ya Fay Herous Fitness amesema yupo tayari kuandaa pambano hilo ili kuondoa ubishi kati ya Mkali Wenu na Mlela.


“Nitazungumza na Mkali Wenu nina imani atakubali kwa sababu anahitaji fedha, hivyo baada ya kumaliza mazungumzo hayo nitawasainisha wote wawili kucheza na kuonyesha ubabe wao."





Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini