WAREMBO 20 kutoka Kanda na Mikoa mbalimbali wa Shindano la Miss Tanzania watarajiwa kuingia kambini ambapo maudhui ya Shindano hilo linatarajiwa kuruka Mubashara Julai 26,2023 st bongo kwenye King'amuzi cha Startimes.
Akizungumza na Wanahabari Leo Mei 31,2023 Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa amesema kwa mara ya pili mfululizo wanaendelea kuunga mkono Shindano hilo la urembo ambapo linawapa nafasi wasichana kutimiza ndoto zao kupitia tasnia ya urembo.
"Jukwaa la urembo limekuwa likifungua fursa mbalimbali kwa warembo hivyo kampuni ya Startimes itaendelea kutoa mchango kwa warembo hao ambapo mara nyinyi wamekuwa wakisaidia jamii zao kupitia talanta zao."
Pia amesema wadau wa urembo wategemee vingi kwenye msimu mwengine wa shindano kwani warembo watakaa kambini kwa wiki 2 na shughuli zao kambini zitakuwa zikiruka mubashara kupitia chaneli ya St bongo King'amuzi cha Startimes.
Hata hivyo ameongeza kuwa Zawadi ya Mshindi wa Miss Tanzania itakuwa kubwa mara 100 zaidi na kuwataka mashabiki waendelee kutazama matukio mbalimbali pindi warembo watakapowasili kambini.
Nae Mkurugenzi wa Uendeshaji wa St bongo Ramadhan Msemo amesema Jukwaa hilo la Miss Tanzania limekuwa likiwakwamua na kuwanyanyua wasichana mbalimbali huku akitoa mfano Mrembo wa Miss Tanzania 2022 Halima Kopwe alivyopata fursa mbalimbali kupitia taji lake na kwa sasa Mrembo huyo anatarajia kuiwakilisha Tanzania kwenye Mashindano ya dunia (Miss world) katika Falme za Kiarabu (Dubai) mwezi Octoba.
"Kupitia udhamini wetu na kuona wasichana wana nafasi katika jamii na wapewe nafasi mrembo Halima Kopwe anaenda kuwa kielelezo tosha cha kuiaminisha jamii zilizotuzunguka kuwa urembo sio uhuni."
Amesema watazamaji wategemee Maudhui mengi kutoka kambini yenye ubora wa hali ya juu huku akiwaomba mashabiki kulipia ving'amuzi vyao mapema kuepuka kupitwa na shindano hilo.
Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Azama Mashango amesema baada ya kanda,vyuo na mikoa kumalizika vizuri sasa ni zamu ya Shindano kubwa la Miss Tanzania ambapo tayari mchujo umekwisha fanyika kupitia Kamati ya Miss Tanzania na takribani warembo 20 wamekidhi vigezo vyote.
Tutegemee warembo wenye vigezo vyote,nidhamu na nembo kwa taifa la Tanzania kupitia tasnia ya urembo na warembo ambao watakula kiapo kusaidia jamii zao katika sekta mbalimbali. "
Pia ametolea ufafanuzi swala la crown( taji) itaendelea kuwa ile ile ambayo mrembo Halima Kopwe 2022 alivalishwa na Kamati ya Miss Tanzania haina ulazima wa kutafuta mpya na wala hakuna masharti yanayodai kuwa mrembo kupewa mpya.
Huku Miss Tanzania 2022 Halima Kopwe amesema atakuwepo kambini kuwafua warembo hao huku akiwaomba watanzania kumpa sapoti ya hali na mali kuelekea mashindano ya urembo kidunia (Miss world ) ambapo mwaka huu yatafanyika falme za Kiarabu (Dubai)

Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa akizungumza na Wanahabari Leo Mei 31,2023 na kueleza namna Kampuni ya Startimes kwa kushirikiana na kampuni ya The look ilivyojipanga kuhakikisha shindano hilo linafanyika huku Startimes ikiwa mdhamini mkuu kwa mara ya pili mfululizo.

Mkuu wa Uendeshaji wa St bongo Ramadhan Msemo akizungumza na Wanahabari Leo Mei 31,2023 na kueleza kwa namna maudhui yatakayoruka ya shindano la Miss Tanzania litaanzia kambini ambapo warembo hao 20 wataingia kambini julai 23,2023 na matukio mbalimbali yataonyeshwa kupitia st bongo hadi kufikia fainali ya shindano hilo.

Miss Tanzania 2022 Halima Kopwe akizungumza na Wanahabari na Leo Mei 31,2023 mara baada ya Uzinduzi wa Shindano la Miss Tanzania na kuwaomba wadau wa urembo kumshika mkono kuelekea mashindano ya urembo dunia (Miss world) yanayotarajiwa kufanyika falme za Kiarabu (dubai) mwezi Octoba 2023.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA



0 Comments