WAZIRI PINDI CHANA MGENI RASMI”LUGALO LADIES OPEN 2023”. | ZamotoHabari

Na.Khadija Seif,Michuzi blog

WAZIRI wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Pindi Chana anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Shindano la “Lugalo Ladies Open 2023” litakalofanyika Mei 20 na 21 Viwanja vya Lugalo Gofu Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Wanahabari  leo Mei 17,2023  Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)amesema,shindano hilo litashirikisha Wachezaji wa Klabu za Gofu Tanzania nzima hasa Wanawake ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Pindi Chana.

"Kutokana na upekee wa shindano hili haswa kuhusisha wachezaji Wanawake tumeona inafaa zaidi Mgeni rasmi awe Mwanamke na kwa bahati nzuri ndio mwenye dhamana ya Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Pindi Chana ndie tumemkusudia kufunga mashindano hayo. "

Hata hivyo amesema Klabu ya lugalo inazidi kuimarika na kukuwa siku hadi siku na kuwa na idadi kubwa ya wachezaji wakike na kupelekea kuwepo kwa shindano hilo.

"Klabu yetu ina takribani wanachama 212 na Wanawake 46 ili kuwapa nafasi Wachezaji Wanawake kuonyesha ujuzi wao."

Kwa upande wake Meneja Masoko wa Benki ya Exim Kauthari D’Souza  ambao ni Wadhamini  Wakuu wa Shindano hilo amesema,Mwanamke anamchango Mkubwa katika Michezo na wao  wanafuraha kuwa sehemu ya Shindano hilo,na wanawaomba Watanzania hasa Wanawake wajitokeze kwa wingi kushiriki shindano hilo.

"Tunafurahi kuwa sehemu ya Shindano hili na tunaunga mkono katika Michezo kwani inachochea uzalendo. "

Pia ameongeza kuwa benki hiyo itaendelea kuunga mkono Michezo mbalimbali na kuungana na Wanawake wote katika kuhakikisha Maendeleo kwa jamii.

Nahodha wa Klabu hiyo kwa Upande wa Wanawake Hawa Wanyeche amesema Shindano hilo linafanyika kwa mara ya tatu mfululizo na mwaka huu litatumika kupata wachezaji watakao iwakilisha Tanzania katika Mashindano ya “East and Central Challenge Trophy”ambalo linalotarajiwa kufanyika  Rwanda Novemba 11 mwaka huu.

"Ni mara ya 3 mfululizo kufanyika kwa shindano hili hivyo inapelekea mchezo huu kuongeza wachezaji wengi na hata hivyo shindano hilo litasaidia zaidi kupatikana kwa wachezaji wa timu ya taifa ya gofu."

Shindano hilo la “Lugalo Ladies Open 2023” Litafanyika Mei 20 na 21 katika Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Lugalo,ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Pindi Chana,huku wachezaji kutoka klabu mbalimbali  za Gofu zitashriki ikiwemo Dar Gymkhana,Arusha Gymkhana pamoja na TPC Moshi Golf Klabu. 


Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)akizungumza na Wanahabari Leo Mei 17,2023 akisisitiza kuwa shindano hilo litashirikisha Wachezaji wa Klabu za Gofu Tanzania nzima hasa Wanawake 

Meneja Masoko wa Benki ya Exim Kauthari D’Souza  ambao ni Wadhamini  Wakuu wa Shindano  la  “Lugalo Ladies Open 2023” .akizungumza na waandishi wa habari leo Mei  17,2023 kuelekea shindano hilo litakalofanyika Mei 20 na 21 Viwanja vya Lugalo Gofu Jijini Dar es Salaam


Nahodha wa Klabu ya Lugalo gofu kwa upande wa Wanawake Hawa Wanyeche akizungumza na Wanahabari Leo Mei 17,2023 kuhusu Shindano la “Lugalo Ladies Open 2023” litakalofanyika Mei 20 na 21 Viwanja vya Lugalo Gofu Jijini Dar es Salaam akiwakaribisha wanamichezo mbalimbali na vilabu vyote vya gofu Tanzania nzima.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini