YANGA SC BINGWA LIGI KUU SOKA TANZANIA BARA 2022-2023 | ZamotoHabari

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Wananchi baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Dodoma Jiji FC kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam rasmi wametangaza ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC PL) ikiwa ni mara ya 29 katika historia ya timu hiyo.

Mabao ya Yanga SC yalifungwa na Mshambuliaji Kennedy Musonda, Mudathir Yahya Abbas (mabao mawili) na Farida Mussa Maliki wakati mabao ya Dodoma Jiji FC yakifungwa na Collins Opare na Seif Karihe.

Katika mchezo huo, Yanga SC walihitaji alama tatu pekee kutwaa ubingwa wa mashindano hayo ya Ligi Kuu, kwa sasa Wananchi wamefikisha alama zao 74 wakiwa na michezo 28 na kubaki na michezo miwili pekee ya kukamilisha ratiba ya Ligi hiyo.

Alama 74 hazitaweza kufikiwa na timu yoyote inayoshiriki Ligi hiyo hata Simba SC wana alama 67 na michezo 28, hawatafika alama hizo hata kama watashinda michezo yao miwili iliyobaki katika Ligi hiyo ya NBC.

Hata hivyo, Ruvu Shooting FC tayari imeshuka daraja kwenye Ligi hiyo, na huenda ikaungana na Polisi Tanzania FC au timu nyingine yoyote wakati nafasi ya kujiuliza kucheza ‘Play Off’ ikiwa bado haijafahamika kwa timu karibu sita ambazo zipo kwenye uwezekano wa kucheza ‘Play Off’.

Timu hizo ni Tanzania Prisons SC, Dodoma Jiji FC, Coastal Union FC, Mbeya City FC, KMC FC na Mtibwa Sugar FC.







Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini