Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Matajiri wa Chamazi, jijini Dar es Salaam, Azam FC wameanza kazi kubwa ya kupanga na kupangua Kikosi chao kuelekea msimu ujao wa mashindano wa 2023-2024 baada ya kuachana na baadhi ya Wachezaji wake na baadhi ya Wataalamu wa Benchi la Ufundi.
Hivi karibuni, Azam FC walitangaza usajili wa Mchezaji mmoja pekee wa ndani, baada ya kutangaza kumsajili Kiungo wa Kimataifa wa Tanzania, Feisal Salum (Feitoto) baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumaliza mtafaruku wake na Klabu yake ya zamani ya Young Africans SC.
Kuelekea msimu ujao wa mashindano (2023-2024) Azam FC wametangaza kuachana na Wachezaji raia wa Zimbabwe, Bruce Kangwa Amaruce (Mlinzi wa Kushoto), Mshambuliaji Rodgers Kola (Zambia), Kiungo Kenneth Muguna (Kenya), Mshambuliaji Ismail Kader (Tanzania) na Kiungo Mshambuliaji Cleophace Mkandala (Tanzania).
Pia, Azam FC imetangaza kuachana na baadhi ya Wataalamu wa Benchi la Ufundi, Kaimu Kocha Mkuu Kali Ongala, Kocha wa Makipa, Dani Cadena (Hispania) na Mtaalamu wa mazoezi ya viungo (Fitness Coach), Dkt. Moath Hiraoui (Tunisia).
Hata hivyo, Azam FC wanaweka sawa Kikosi chao ambacho kinatarajiwa kucheza Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) msimu ujao wa mashindano.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA




0 Comments