Na.Elimu ya Afya kwa Umma.
Ikiwa Bonanza la Afya lilioandaliwa na Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais TAMISEMI likiendelea katika maeneo mbalimbali Kwa mikoa mitano hapa nchini, kwa Mkoa wa Dodoma Bonanza hilo limefika katika chuo Kikuu cha St.John na Chuo Kikuu cha Dodoma.
Wakizungumza katika Bonanza hilo, baadhi ya wanachuo kutoka chuo Kikuu cha St.John pamoja na Chuo Kikuu cha Dodoma wamesema Bonanza hilo limekuwa na tija kwao kwani wamepata fursa ya kupima Afya zao,elimu ya lishe, Afya ya Uzazi ,Afya ya akili, kupima uzito, elimu ya ukatili ,umuhimu wa mazoezi pamoja na elimu juu ya Virusi vya UKIMWI.
"Wizara ya Afya imetufikishia Bonanza hili tumenufaika sana kwani tumepata wasaa wa kupima afya zetu pia mazoezi yanajenga afya natoa wito Kwa wengine waendelee kujitokeza"amesema Laimu Nuru kutoka Chuo Kikuu cha St.John.
"Hakika nimepata vingi kutokana na Bonanza hili kwanza nimeelezwa umuhimu wa lishe bora, namna ya kuchukua tahadhari dhidi ya mimba zisizotarajiwa sisi watoto wa kike tuwapo chuoni,elimu ya ukatili, kupima uzito"amesema mmoja wa wanafunzi kutoka chuo Kikuu cha Dodoma.
Katika Bonanza hilo Mkoani Dodoma Juni 16,2023 jumla ya Wanafunzi 420 Chuo Kikuu cha Dodoma wamefikiwa na elimu ya afya na kupima afya zao, Chuo Kikuu cha St.John kukiwa na Wanafunzi 256 wakipata elimu hiyo .
Halikadhalika waliopima hali ya lishe Juni 16,2023 ni watu 97,waliojitokeza kupata elimu juu ya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza na kupima ni watu 75 na jumla ya watu waliojitokeza kupima Virusi vya UKIMWI ni 143 Hadi kufikia Juni 16,2023.
#Elimu ya Afya kwa Umma.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments