FURAHISHA, HAMADI MBABE KUJULIKANA AGOSTI O4 | ZamotoHabari

Na.Khadija Seif, Michuziblog
MABONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Hamadi Furahisha na Kassim Hamadi wanatarajia kupigana katika pambano la 'Usikae Kinyonge' litakalofanyika Agosti 4 mwaka huu, Dar es Salaam.

Furahisha na Hamadi watacheza pambano la kuwania mkanda wa Ubingwa wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) la raundi 10 uzito wa Kati.

Akizungumza na Wanahabari Leo Julai 26,2023  Jijini Dar es salaam  Promota wa pambano hilo, Abdul Salimu amesema bingwa atayeshinda katika pambano hilo atatafutiwa mpinzani wa kucheza naye kutoka nje ya nchi.

"Kutakuwa na mapambano 16, 13 boxing wakati matatu ya kick boxing, pia mabondia hawa walifanya vyema nitawaandalia mapambano mengine ya kimataifa, "alisema Salimu.

Promota huyo ameeleza pamoja na pambano hilo kutakuwa na mtanange mwingine kutoka kwa Miraji Fundikila 'MkaliWenu' atacheza na Frank John 'Jitu Kali'.

Bondia Furahisha amesema amejipanga kucheza mchezo mzuri siku hiyo na kutoa burudani kutoka kwa wadau ambao watakuwepo.

Furahisha atahakikisha anacheza katika kiwango bora kwa lengo la kushinda mkanda huo.

"Mashabiki na wadau wa masumbwi wategemee mchezo nzuri kutoka kwangu, pia mkanda huu lazima urudi Temeke,"alisema Furahisha.

Hamadi amemtaka mpinzani wake afanye mazoezi ili wacheze mchezo mzuri siku hiyo.

"Wito wangu kwa Furahisha afanye mazoezi ili siku hiyo tuonyeshe mchezo nzuri, pia Mshindi apatikane, "alisema Hamadi."

Hata hivyo pambano hilo litasindikizwa na mabondia ambao ni walinzi (bodyguard) kutoka Kampuni ya Sasec security services ambao wameingia katika mchezo wa Ngumi kama sehemu ya kuonyesha vipaji vyao na kuongeza ukakamavu.





Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini