SAMATTA AIBUKIA UGIRIKI | ZamotoHabari

 

 


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV.


NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Ally Samatta (Samagoal) ametambulishwa na Klabu ya POAK inayoshiriki Ligi Kuu Soka nchini Ugirirki akitokea Klabu ya Fenerbahçe ya Uturuki.

Samatta bado yupo barani Ulaya kulinda kipaji chake cha soka, amesaini mkataba wa miaka miwili na nyongeza ya mwaka mmoja katika Klabu hiyo. Samatta alikuwa Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji alipopelekwa kwa mkopo.

Mwaka 2020, Samatta aliweka historia ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi Kuu Soka nchini Uingereza (EPL) katika Klabu ya Aston Villa. Ambapo alicheza michezo 14 pekee na kufunga bao moja.

Mwaka 2020 hadi 2023 alicheza Fenerbahçe ya Uturuki ambapo alifunga mabao matano pekee katika michezo 30 aliyocheza Klabuni hapo, Samatta alitolewa kwa mkopo katika Klabu ya Royal Antwerp ya Ubelgiji msimu wa 2021-2022.

Msimu wa 2022-2023, Samagoal alirudi tena kwa mkopo katika Klabu ya KRC Genk hadi msimu wa mashindano ulipotamatika, msimu ujao wa 2023-2024 atakuwa na Klabu mpya ya POAK.

POAK FC walimaliza nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Soka nchini Ugiriki msimu uliopita wa 2022-2023, walimaliza nafasi hiyo wakiwa na alama 54 katika michezo yao 26 ya Ligi Kuu. Bingwa wa msimu katika Ligi hiyo alikuwa Panathinaikos FC ambaye alikuwa na alama 61 katika michezo 26.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini