TWAHA KIDUKU APOTEZA PAMBANO NYUMBANI | ZamotoHabari

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

BONDIA wa Ngumi za Kulipwa nchini Tanzania, Twaha Kassim (Kiduku) amepoteza pambano la ubingwa wa WBF Inter Continental dhidi ya Bondia kutoka Afrika Kusini, Asemahle Wellem pambano lililofanyika kwenye ukumbi wa Malaika jijini Mwanza.

Pambano hilo la raundi 12 ilishuhudiwa Twaha Kiduku akipoteza kwa pointi za Majaji wote watatu huku Asemahle akibeba pointi nyingi baada ya kutawala pambano hilo kwa kiasi kikubwa katika raundi zote 12.

Twaha Kiduku mara zote alikuwa anamuwinda mpinzani wake kumpiga ngumi za ushindi ‘Counter Punch’ kwenye kona za ulingo lakini ngumi hizo hazikufanikiwa kwa kiasi kikubwa mbele ya Bondia huyo kutoka Afrika Kusini ambaye mara zote alitumia mbinu za kushika (kukumbatia) pindi anapowekwa kwenye kona za ulingo.

Hata hivyo, haikuwa siku nzuri kwa Twaha kwenye jiji la Miamba (Mwanza) mbele ya mpinzani huyo ambaye pia kutokana na ujanja wake ulingoni, alifanikiwa kumuangusha Kiduku kwenye raundi ya tatu ya pambano hilo baada ya kumpiga ‘Left hook punch’ ya ghafla na kufanya Mwamuzi kumuhesabia.

Wadau mbalimbali wa mchezo wa ngumi wametoa maoni yao kwa pambano hilo huku wakimtia Moyo, Bondia Twaha Kiduku baada ya kupoteza pambano hilo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla na wadau wengine wa mchezo wa Ngumi waliokuwa kwenye burudani hiyo ya vitasa.





Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini