WACHEZAJI TISA KUIWAKILISHA LUGALO MAREKANI | ZamotoHabari

Wachezaji Watakao liwakilisha Jeshi na Nchi katika Mashindano ya Dunia ya Majeshi Santiego Nchini Marekani Oktoba Mwaka huu wakiwa katika Picha ya Pamoja na Uongozi wa Klabu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Lugalo Gofu Dar es Salaam

WACHEZAJI Tisa wa Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Lugalo wanatarajia kuliwakilisha Jeshi na Nchi katika Mashindano ya Dunia ya Majeshi Santiego Nchini Marekani Oktoba Mwaka huu.

Mwenyekiti wa Lugalo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amewataja Wachezaji hao kuwa ni Kapteni Chediel Msechu, Kapteni Samuel Mosha, Marius Kajuna, Samuel Kileo, John Hiza, Nsajigwa Mwansasu na Kwa Wanawake ni Letisia Kapalila, Zumla Hamisi na Hadija Selemani.

Brigedia Jenerali Mstaafu Luwongo amesema Wachezaji waliopata nafasi watashiriki Mashindano ya Mufindi Open, Morogoro Open na kuweka Kambi Jijini Arusha Mwezi wa Tisa lengo ikiwa kurejea na ushindi.

Miongoni mwa Wachezaji waliopata nafasi wamesema,changamoto zilikuwa kubwa viwanjani lakini kupitia mazoezi na kujituma imewawezesha kufanya vizuri.

Mchakato wa Kuwatafuta wachezaji watakaoliwakilisha Jeshi na Nchi katika Mashindano hayo ya Dunia ya Majeshi Mwezi Oktoba Nchni Marekani limehitimishwa Leo hii tayari Kwa ajili ya Kambi.


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini