Warembo wote akiwemo Halima watapokelewa tarehe 8 November kwa ajili ya kuanza kambi rasmi ya msahindano kwa muda wa mwezi mmoja kabla ya fainali
Kama ilivyoutaratibu siku chache kabla ya kuanza safari Miss Tanzania anatarajiwa kukabidhiwa bendera ya Tanzania ili kuagwa rasmi na Waziri wa Habari Tamaduni Sanaa na Michezo
Mbali na kwenda kushindana Miss Tanzania atatumia fursa hii kutangaza utalii na Taifa la Tanzania katika jukwaa la dunia.
Watanzania na wadau wote wa sanaa burudani na michezo wakiwemo wanahabari tuungane kumpa nguvu mwakilishi wetu katika mashindano haya makubwa ya dunia.
Kwa habari zaidi na muendelezo wa matukio yanayojiri yatawekwa kwenye ukurasa rasmi wa Miss Tanzania kwenye mitandao ya jamii @misstanzaniaorganisation
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA




0 Comments