TANZANIA YAJIVUNIA MEDALI YA KWANZA NGUMI KWA WANAWAKE KIMATAIFA | ZamotoHabari


▫️Ni ya Malkia wa Ngumi Grace Joseph Mwakamele

▫️ Apata medali ya Fedha na zawadi ya pesa Usd $10,000

6-8-2023 Yaounde, Cameroon .

Licha ya kupoteza pambano lake la fainali Ubingwa wa Afrika 2023 uzani wa Light middleweight 70kg dhidi ya Bingwa mtetezi na Mshindi wa pili Ubingwa wa Dunia Istanbul 2022 Alicida Panguane kutoka Msumbiji, GRACE JOSEPH MWAKAMELE ameweka historia ya kuwa MWANAMKE WA KWANZA MTANZANIA kushinda medali Kimataifa katika mchezo wa Ngumi katika michezo ya Ubingwa wa Afrika kwa Wanaume na Wanawake Yaounde 2023.

Mwakamele ameshinda medali ya Fedha na zawadi ya pesa Usd $10,000.

Timu ya Tanzania iliyowakilishwa na wachezaji 3 imefanikiwa kuliheshimisha Taifa kwa ushindi wa medali mbili (1 Fedha ya Mwakamele na 1 Shaba ya Yusuf Changalawe)

Tanzania 🇹🇿 ya Mama Samia pia ndio imekua Taifa pekee kuwakilishwa na jinsia ya Kike wengi kuliko wanaume (Wanawake 2 na Mwanaume 1) katika mashindano haya.

Mara ya mwisho kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika ilikua Afrika ya Kusini mwaka 1994.

Imetolewa na:
Ofisi ya Raisi - BFT

Mwakamele kushoto na Mwalimu wa Timu ya Taifa ya Ngumi Samwel Kapungu "Batman" wakifurahia ushindi wa kuingia fainali baada ya kumchakaza Seynabou Ndiaye kutoka Senegal hatua ya nusu fainali.

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini