Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MCHEZO wa fainali ya mashindano ya Ndondo CU umemalizika kwa timu ya soka ya Madenge kuibuka mabingwa baada ya kuichabanga timu ya Kibangu Rangers mabao 2-0 na hivyo kujinyakulia kitita cha Sh.milioni 30.
Fainali ya mashndano hayo imefanyika leo Agosti 3, 2023 katika Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam na kudhuriwa na maelfu ya mashabiki wa soka sambamba na wadau wa michezo nchini.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ndiye aliyekuwa mgeni rasmi ambaye alikabidhi medali, kikombe pamona na kitita cha Sh.milioni 30 kwa mabingwa huku mshindi wa pili Kibangu Rangers wakikabidhiwa medali na fedha Sh.milioni 20.
Naibu Waziri Mwinjuma pia alikabidhi medali kwa waamuzi wote wa michuano hiyo ya Ndondo Cup huku pia akikabidhi fedha kwa mfungaji bora wa michuano hiyo.
Katika mchezo huo wa fainali ambao ulishuhudiwa na maelfu ya mashabiki wa soka walionekana kufurahia fainali hiyo kutokana na timu zote mbili kutumia kasi, mbinu na akili wakati wa mchezo huo.
Hata hivyo timu ya Madenge walionekana kuwa bora zaidi na hivyo kufanikiwa kushinda mabao 2-0 na hivyo kuwawezesha kuwa mabingwa ikiwa ni mara pili mfululizo.
Mashabiki wa timu ya Kibangu Rangers baada ya kufungwa bao 2-0 wengi wao walikata tama na hivyo kuanza kuondoka wakati mchezo unaendelea huku mashabiki wa Madenge wakiamsha shangwe la ubingwa.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA




.jpeg)

.jpeg)



0 Comments