DULLA MBABE KUPANDA ULINGONI PAMBANO LA "SISI NI PIPO" | ZamotoHabari

BONDIA Abdallah Pazi maarufu kama "Dulla mbabe anatarajia kutangaza utalii kupitia mchezo wake wa Masumbwi katika pambano la "sisi ni pipo" ambalo litafanyika Novemba 25,2023 Jijini Arusha.

Akizungumza na Wanahabari Leo Oktoba 23,2023  Promota wa pambano hilo kutoka Kampuni ya Lady in red Sophia Mwakagenda amesema lengo la Pambano hilo ni kutangaza Vivutio vya Utalii vilivyopo nchini Tanzania.

Amesema kutokana na ukubwa wa  mabondia ambao wanacheza siku hiyo utalii wa nchini utazidi kufahamika nje ya mipaka.

"Pambano hili madhubuti kwa ajili  ya kutangaza utalii wa ndani, ndiyo maana tumepeleka Arusha, pia kuendeleza vipaji vya vijana wetu."

Promota huyo ameeleza kuwa kutakuwa na mapambano mawili ya wanawake kwa ajili ya kuonyesha uwezo wao.

Bondia, Dullah Mbabe amesema amejipanga vyema kuhakikisha analipiza kisasi kutoka kwa mpinzani wake, Katompa.

"Kabla mwaka kuisha bondia Kamtopa nilikua namtaka sana ili tuweze kumaliza kisasi chetu hii sasa ndio fursa kwangu na mashabiki wangu kuona nalipa kisasi hiki Arusha".

Hata hivyo amebainisha kuwa ni kwa mara ya kwanza anaenda kutembelea vivutio vya utalii na fursa ya kipekee kama mzalendo na Mtanzania kutumia kipaji chake (Masumbwi) kutangaza Utalii kama alivyofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu kupitia Filamu ya "Royal tour ".

Mbali na pambano la Dulla mbabe na Katompa mabondia wengine watakaopanda ulingoni ni Shaban Kaonek,Lauren Japhet, Jacob maganga na wengine wengi.




Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini