"NCBA BANK TANZANIA OPEN 2023 KUTIMUA KIVUMBI KILI GOLF | ZamotoHabari

MASHINDANO ya Wazi ya Mchezo wa Gofu "NCBA BANK TANZANIA OPEN 2023" yanatarajiwa kuanza rasmi Novemba 23 Hadi 26 Mwaka huu katika Klabu ya Kili Golf Jijini Arusha.

Akizunguza na Wanahabari Jana Oktoba 24,2023 Mwenyekiti wa Chama Cha Mchezo wa Gofu Tanzania (TGU) Girman Kasiga amesma Shindano Hilo litajumuisha Wachezaji zaidi ya 200 kutoka Klabu za ndani ya nchini na nchi Jirani Kama Ethiopia,Kenya,Uganda na Afrika kusini.

"Shindano hili tumelitaka liwe kubwa zaidi ili kuwapa motisha wachezaji wa gofu nchini Tanzania kuongeza ufanisi katika mchezo huo na kuona viwango vyao hivyo tumeshirikisha Wachezaji kutoka mataifa mbalimbali sio tu kushindana bali pia kujenga mahusiano mazuri yenye tija kupitia michezo ."

Hata hivyo Kasiga ameeleza mpaka sasa muitikio wa shindano hilo limekuwa mkubwa kutokana na Wachezaji kuendelea kujisajiri kushiriki shindano hilo kubwa.

Pia ametoa wito kwa Makampuni na taasisi nyingine kujitokeza kudhamini shindano hilo huku akiweka wazi kama Chama cha michezo (TGU) Kuweka jitihada za kuhakikisha Wachezaji watoto (JR) Wanapewa Kipaumbele cha kufanya vizuri na kutimiza ndoto zao.

Kwa upande wake mdhamini mkuu wa shindano hilo Claver Serumaga Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NCBA amesma Wamejipanga kikamilifu kudhamini Shindano Hilo "NCBA BANK TANZANIA OPEN 2023".

"Taasisi yetu ya kibenki ambayo pia ipo katika nchi za Afrika Mashariki imekuwa ikiandaa mashindano ya Gofu ya NCBA kwa mwaka wa nne nchini Kenya na Uganda ikiwa kwa mara ya pili na safari hii imeamua kutambulisha mashindano hayo nchini Tanzania ili kuendelea kurudisha kwa wateja wake kupitia sekta mbalimbali lakini hususani sekta ya michezo. "

Pia ameeleza kuwa kuna zawadi mbalimbali ambazo washindi watapatiwa katika shindano hilo kutoka benki ya NCBA ambapo washindi pia watapata nafasi ya kushiriki mashindano makubwa disemba mwaka huu nchini Kenya.

"Washindi wa Shindano Hilo la "NCBA BANK TANZANIA OPEN 2023" Wataiwakilisha Tanzania Katika Mashindano Makubwa ya Mchezo wa Gofu Desemba Mwaka huu Nairobi Kenya.
 

Mwenyekiti wa Chama Cha Mchezo wa Gofu Tanzania  Girman Kasiga  akipokea Hati ya mkataba kutoka kwa wadhamini wa Shindano la  "NCBA BANK TANZANIA OPEN 2023" Kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NCBA  Claver Serumaga ambao ndio wadhamini wakuu washindano hilo linalotarajiwa kufanyika Novemba 23,2023 hadi Novemba 26,2023 Jijini Arusha



Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini