KAMPUNI ya Meridianbet imeadhimisha siku ya Utu duniani kwa namna ya tofauti baada ya kufika Kigamboni na kutoa msaada wa mahitaji muhimu kwa familia za hali ya chini mapema leo.
Kampuni hiyo imeangalia namna ambayo inaweza kuadhimisha siku hii na njia pekee wameona ni kuzigusa zile familia ambazo hazijiwezi, Ambapo wametoa msaada wa mahitaji kama Sukari, Unga, Mchele, Mafuta, na Sabuni.
Meridianbet wameyafanya hayo katika kuuadhimisha siku ya Utu duniani ambayo hufanyika kila mwaka Agosti 19, Hivo wao wamehakikisha wanarejesha kwenye jamii ambazo zina uhitaji ili kwenda sambamba na wiki hii ya Utu duniani.
Bado mabingwa wa michezo ya kubashiri Meridianbet wanaendelea kuhakikisha unapigwa mkwanja wa kutosha kupitia michezo mbalimbali inayopigwa haswa baada ya EPL kurejea ambapo wanaendelea kumwaga ODDS BOMBA kila siku.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko kutoka Meridianbet Bi Nancy Igram aliongoza zoezi hilo na kufanikiwa kuzungumza machache “Kama inavyofahamika leo tunaadhimisha siku ya Utu duniani na sisi tumeamua kuuonesha Utu wetu kwenu na ndio maana tumefika hapa leo kujumuika na nyie kwa kutoa mahitaji haya muhimu kwenu”
Aidha familia ambazo zimeweza kupokea msaada leo kutoka kwa Meridianbet hazikuacha kutoa shukrani kwa mabingwa hao wa michezo ya kubashiri na kusema makampuni, taasisi zingine zinapaswa kufanya kama ambavyo wamefanya Meridianbet kwa kuzikumbuka jamii zenye uhitaji.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments