KUAMBIANA CUP YAHITIMISHWA- DC LUDEWA ATUMA UJUMBE KWA VIJANA | ZamotoHabari

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Olivanus Thomas amewataka wachezaji wa timu ndogo ndogo za mitaani kutumia vyema fursa wanazozipata kutoka kwa wafadhili ikiwemo kupelekwa katika Academy mbalimbali ambapo wanapaswa kuwa wavumilivu kwenye academy hizo Ili waweze kutimiza malengo yao.

Mkuu huyo wa Wilaya ameyasema hayo alipokuwa akihitimisha mashindano ya Kuambiana Cup na kuongeza kuwa vijana wengi wanataka mafanikio ya haraka haraka pasipo kuwa na uvumilivu kwa hatua wanazopitia kitu ambacho kinawapelekea kukata tamaa njiani na ndoto zao kuishia njiani.

Aidha Kwa upande wake Mwandaaji wa mashindano hayo Imani Haule almaarufu kama Kuambiwa amesema mara kadhaa katika uendeshaji wa ligi hiyo wamekuwa wakiwachukua vijana kwenda kuwapeleka katika Academy mbalimbali lakini wengine wamekuwa wakiishia stendi na kutaka kurudi huku wengine wakivumilia Kwa muda kadhaa na kushindwa.

"Ligi ya msimu huu tumepata vijana wanne ambao nitaondoka nao kwenda kuwaendeleza vipaji vyao, Ili wasiishie njiani kama walivyovyafanya wenzao hapo awali tutaonana na familia zao na kuwaomba tuzungumze kwa pamoja na vijana wao Ili walifika huko wawe wavumilivu na kutoishia njiani".








Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini