WABABE WAANZA VIZURI LIGI KUBWA ULAYA | ZamotoHabari



WABABE kadhaa katika ligi tano bora barani ulaya wamefanikiwa kuanza vizuri katika ligi zao, Vilabu vya Barcelona, Man City, Liverpool, Inter Milan, Bayern Munich, na PSG wameanza kwa mguu wa kulia michezo yao ya awali kwenye ligi zao.

Liverpool haikudhaniwa kuanza msimu vizuri kwani waliondokewa na kocha wa Jurgen Klopp wengi wakiamini inaweza kuwachukua muda kujipata, Lakini imekua tofauti kwani mpaka sasa wameshinda michezo yao mitatu chini ya kocha Arne Slott na kucheza mpira wa kuvutia kwelikweli.

Ligi kuu ya Hispania Barcelona wao wamekuja kitofauti chini ya kocha Hans Flick kwani wameonekana kucheza mpira mzuri lakini pia wanatoa dozi kubwa kwa wapinzani, Mpaka sasa wameshinda michezo yao yote mitatu ya mwanzo huku wakifunga mabao mengi, Wapinzani wao Real Madrid hali imekua tofauti kwani wametoa sare michezo miwili kati mitatu.

Kunako ligi kuu ya soka nchini Ufaransa PSG mabingwa watetezi nao wameonekana kuanza kwa kasi na kuhitaji kutetea taji lao kikamilifu, Kwani kwenye michezo mitatu ya awali wameshinda michezo yote, Huku klabu ya Olympique Marseille wakiwafata kwa ambao wameshinda michezo yao miwili kati ya mitatu na kusare mchezo mmoja.

Ligi kuu ya soka nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga haijaanza vizuri kwa mabingwa watetezi wa Bayer Leverkusen ambao walimaliza msimu bila kupoteza mchezo wowote, Lakini msimu huu tayari wameshapoteza mchezo mmoja kati ya miwili waliyocheza huku wapinzani wao Bayern Munich wakishinda michezo yao yote miwili.

Seria A ligi kuu ya soka nchini Italia nayo imeanza kurindima ambapo mabingwa watetezi klabu ya Inter Milan imeanza vizuri msimu kwani inaongoza msimamo wa ligi hiyo mpaka sasa wakiwa na alama 7 kwenye michezo mitatu wakifungana na Juventus ambao nao wameanza msimu vizuri.

Endelea kufurahia kubashiri na Meridianbet mabingwa wa michezo ya kubashiri ambao wanatoa ODDS BOMBA kuliko sehemu yeyote ile, Lakini pia machaguzi mengi zaidi ya 1000 Bashiri sasa michezo itakayopigwa wikiendi hii uweze kupiga mkwanja.

Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini