BSS MSIMU WA 15 WAZINDULIWA RASMI | ZamotoHabari

SHINDANO la kusaka Vipaji Tanzania Bongo Star Search 'BSS' misimu wa kumi na tano umezinduliwa rasmi kwa sasa ni Bongo Star Search African wanavuka boda.

Akizungumza na wakati wa uzinduzi wa misimu huo mpya Mkurugenzi Mkuu wa Benchmark 360 Limited Rita Paulsen amesema kuwa Msimu huu wa kumi na tano wa Bongo Star Search ni wa kipekee sana, na ni wa kihistoria.

"Kwanza kabisa, napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mungu na kuwashukuru wote mliojitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hii kubwa, uzinduzi wa msimu mpya wa Bongo Star Search Afrika.

"Kwa miaka mingi tumeweza kuibua vipaji kutoka Tanzania pekee, lakini msimu huu tunaingia hatua nyingine ya juu kabisa.

"Kwa mara ya kwanza, tunavuka mipaka ya nchi, tukifanya usahiri katika nchi zaidi ya tano, zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, na Congo.

"Lengo letu kuu ni kufungua fursa kwa vijana wengi zaidi kutoka ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati, kuwapa jukwaa la kuonesha vipaji vyao na kuendeleza ndoto zao.

Amesema kuwa Muziki ni lugha ya ulimwengu, na tunataka kuwapa wasanii chipukizi kutoka sehemu mbalimbali nafasi ya kuungana na kuunguruma kwenye jukwaa hili kubwa.

"Msimu huu, kama mlivyosikia, utakua ni mkubwa zaidi kuwahi kutokea. Tumeweka mipango madhubuti kuhakikisha kuwa sio tu tunaboresha uzoefu wa mashindano, lakini pia tunapandisha kiwango cha ubora katika kila hatua.

"Tutakuwa na majaji wa kimataifa,
waelimishaji wenye uzoefu, na wasanii waliobobea watakaoshirikiana na washiriki wetu ili kuhakikisha kuwa wanapata elimu ya juu na mwongozo sahihi wa kimasoko na kisanii.

Aidha ameongeza kuwa Kikosi kazi cha majaji watakao jaji msimu wa kumi na tano Jaji Mkuu Ritha Paulsen 'Madam Ritha',Johakim Kimario 'Master J' Jaji
Produza S2KZ ZOMBI Jajitanzania Salama Jabiri SalamaJ Jajitanzania lakini kutakuwa na majaji wawili watakao jaji kutoka nchini Kenya Jaji Sanaipei Tande na Jaji Lilian Mbabazi kutokea Uganda

"Watangazaji watakao sherehesha msimu wa kumi na tano ni Idris SultanIdris Mshehereshaji wa Kipindi pamoja na Meena Ally 'Meena Ally' Mshehereshaji wa Kipindi

Madam Rita ameongeza kuwa "Washiriki wetu, nataka kusema kuwa huu ni wakati wenu.Hii ni nafasi ya kipekee ambayo inaweza kubadilisha maisha yenu."alisema Madam Ritha

Pia ameongeza Ushiriki wenu sio tu katika mashindano, bali ni safari ya kujifunza, kukua, na kufikia malengo yenu makubwa. Hivyo basi, jiandaeni, amini katika vipaji vyenu, na wekeni juhudi kubwa katika kila hatua.

"Kwa wadhamini wetu na washirika wa Bongo Star Search, tunatoa shukrani.
Hamjawa tu wadau, bali ni sehemu muhimu ya mafanikio ya mpango huu. Ushirikiano wenu umetufanya kufikia malengo haya ya kupanua wigo na kufikia zaidi ya mipaka ya Tanzania.

Mashindano hayo yataonyeshwa kupitia vyombo mbali mbali vitakazo kuwa vinaonesha kipindi chetu moja kwa moja Tanzania: St Swahili Channel ndani ya Star Times Uganda: Makula Tv Nairobi: St Swahili ch 160 & 400


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini