MSIMAMO wa ligi kuu ya Uingereza mpaka sasa unaongozwa na majogoo kutoka Anfield klabu ya Liverpool, Lakini wapinzani wao wa karibu vilabu vya Arsenal pamoja na mabingwa watetezi klabu ya Manchester City wakiwafukuzia kwa karibu.
Liverpool ambao wamecheza michezo saba mpaka sasa wanaongoza msimamo wa ligi hiyo pendwa duniani kwa alama 18, Kwani wamefanikiwa kushinda michezo sita na kupoteza mchezo mmoja katika michezo saba ambayo wameshakwisha kucheza.
Klabu hiyo haikudhaniwa kua inaweza kua na mwanzo mzuri msimu huu kutokana na kuondoka kwa aliyekua kua kocha wao Mjerumani Jurgen Klopp, Lakini hali imekua tofauti kwani wamefanikiwa kuanza msimu vizuri chini ya kocha mpya Arne Slot.
Wakati huo vilabu vya Arsenal pamoja na Manchester City havipo mbali kwani na wao wanawafukuza Liverpool kwa karibu kupitia michezo saba ambayo na wao wamecheza, Kwani wao wamekusanya alama 17 kila mmoja wakiwa nyuma ya vinara kwa alama moja.
Endelea kufurahia kubashiri na Meridianbet mabingwa wa michezo ya kubashiri ambao wanatoa ODDS BOMBA kuliko mahala pengine, Lakini pia machaguzi mengi zaidi ya 1000 Bashiri sasa michezo itakayopigwa wikiendi hii uweze kupiga mkwanja.
Mpaka sasa vita inaonekana bado mbichi kwenye ligi hiyo kwani kiongozi wa msimamo wa ligi hiyo ambaye ni klabu ya Liverpool yupo kileleni kwa alama akiwa na alama 18, Huku Arsenal na Man City wakiwa na alama 17 wakiwa wamecheza michezo 7 kila mmoja.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments