KAMPUNI bingwa ya kuchapisha makala ya michezo Mtandaoni Meridiansports imefanikiwa kutoa na kurudisha kwenye jamiii kwa mara nyingine ambapo leo wamefika kwenye Shule ya Sekondari Jangwani na kutoa msaada kuendeleza desturi yao ya miaka mingi.
Huu umekua utaratibu wa Meridiansports miaka na miaka kuhakikisha wanawapatia kile kidogo wanachopata pamoja na jamii yao.
Zoezi hili ni sehemu ya kampeni ya Meridiansports ya kusaidia afya na elimu kwa watoto wa kike kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata mahitaji muhimu ya kiafya yanayowawezesha kuhudhuria masomo yao bila vikwazo. Taulo za kike ni mahitaji muhimu kwa wasichana shuleni, na ukosefu wake unaweza kuwa changamoto kwa mahudhurio na maendeleo yao ya kitaaluma.
Kikawaida Meridiansports wamekua wakijitahidi kurudisha kwa jamii yake na hua wanarudisha pale ambapo kuna uhitaji mkubwa, Kama ambavyo shule ya Sekondari Jangwani imefikiwa kwakua imeonesha kukidhi vigezo na ni wazi wasichana wa shule hiyo walikua na uhitaji mkubwa wa mataulo ili kuweza kuimarisha mazingira yao ya kiafya.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Muhariri kutoka Meridiansports, Bi. Nancy Ingram, alisema, “Tunatambua umuhimu wa elimu kwa kila mtoto wa kike na changamoto wanazokumbana nazo wanapokosa vifaa muhimu vya usafi wa kibinafsi. Hii ndiyo sababu Meridiansports inajitahidi kusaidia jamii kwa kuhakikisha wasichana wanapata msaada wanaohitaji ili waweze kusoma bila changamoto.”
Meridiansports imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia jamii kupitia miradi mbalimbali ya kijamii, ikiwa ni pamoja na elimu, afya, na mazingira. Kampuni hiyo inaendelea kutekeleza programu zake za uwajibikaji wa kijamii ili kuhakikisha jamii inafaidika kwa njia endelevu.
Aidha Mwakilishi kutoka shule ya Jangwani Sekondari, aliishukuru Meridiansports kwa msaada huu muhimu na kueleza kuwa, “Msaada huu utasaidia kupunguza changamoto wanazokutana nazo wanafunzi wetu wa kike. Tunawashukuru Meridiansports kwa kuona umuhimu wa kusaidia wasichana wa shule yetu.”
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA
0 Comments