SIKU ya kuacha njumu uwanjani imefika ambapo wababe wa Kimataifa kushuka dimbani hapo baadae kusaka pointi 3 za uhakika. Je nani unamuona ataondoka kidedea?
Leo hii utapigwa mchezo wa Kundi D wa kufuzu michuano ya AFCON 2027 kati ya Eritrea dhidi ya Afrika Kusini huku timu zote mbili ukiuangalia mchezo huu kwa jicho tofauti sana kwani wote wawili wanahitaji kupata ushindi mnono hapa.
Afrika Kusini inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na pointi 3 baada ya kuifunga Guinea kwa mabao 2-1, huku Eritrea wao walianza kampeni yao i kwa kupata sare ya 1-1 dhidi ya Kenya mjini Nairobi.
Kwa kuwa Kenya ni mwenyeji mwenza wa AFCON 2027 na tayari ina nafasi ya kushiriki fainali, ni timu moja tu kati ya Afrika Kusini, Guinea na Eritrea itakayofuzu kutoka kundi hilo hivyo kila pointi katika michezo hii ina uzito mkubwa.
Kwa Eritrea, sare dhidi ya Kenya ilikuwa matokeo yaliyowapa nguvu kubwa kisaikolojia. Kenya ililazimika kusubiri hadi dakika ya 87 kusawazisha goli hilo. Hii inaonyesha kwamba Eritrea si timu inayopaswa kuangaliwa kwa ukubwa wa jina pekee. Bashiri hapa.
Je unajua kuwa kuna baadhi ya wachezaji watakosekana kwenye mechi hizo?. Basi kwa taarifa zaidi ingia Meridianbet na kule utajua ni nani na nai hayupo lakini pia kujua misimamo ya makundi mbalimbali.
Lakini changamoto yao sasa ni kubwa zaidi kwa sababu wanakutana na Afrika Kusini ambayo tayari imeonyesha uwezo wa kupambana hadi dakika za mwisho. Ushindi huo ulimpa kocha Pitso Mosimane mwanzo wa ushindi katika awamu yake mpya ya kuiongoza timu ya taifa.
Afrika Kusini inaweza kuwa na faida ya kisaikolojia kwa sababu imeanza kampeni kwa ushindi dhidi ya mmoja wa wapinzani wake wakuu wa kundi. Lakini mchezo wa Eritrea utakuwa tofauti. Guinea ilicheza kwa ujasiri na kuilazimisha Bafana Bafana kufanya kazi kwa nguvu, wakati Eritrea inaweza kuwa na mpango wa kujilinda kwa kina zaidi na kusubiri muda sahihi wa kushambulia.
Kwa hiyo, Eritrea haitahitaji kuingia kwenye mchezo wa kushambuliana bila mpangilio. Itahitaji kuwa na subira, kulinda eneo la mbele ya mabeki na kuhakikisha kwamba kila mpira wanaoupata wakati wa kuvunja mashambulizi ya Afrika Kusini unatumiwa kwa ufanisi.
Eneo la kiungo linaweza kuwa sehemu muhimu zaidi ya mchezo huu. Afrika Kusini ikifanikiwa kutawala kiungo, kusogeza mpira kwa kasi na kuwafanya wachezaji wa Eritrea kurudi nyuma, inaweza kutumia muda mwingi ikiwa kwenye nusu ya uwanja ya mpinzani.
Pia Eritrea ikifanikiwa kukata njia za pasi na kuzuia Afrika Kusini kupata nafasi kati ya mistari, mchezo unaweza kuwa wa kusubiri sana. Hapo ndipo Afrika Kusini itahitaji uvumilivu kwa sababu kulazimisha pasi za hatari kunaweza kuipa Eritrea nafasi ya kushambulia kwa kushtukiza.
Ukiingia Meridianbet unaweza ukaziona mechi zote kwa ukubwa zaidi na kujua nani na nani wanacheza leo.
Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA




0 Comments