Harry Kane Kwenye Kinyang’anyiro cha Ballon d’Or | ZamotoHabari


TUZO za Ballon d’Or zimezidi kupamba moto huko Ulaya huku Harry Kane akiwa ni moja ya wachezaji ambao anapigiwa upatu wa kuchukua tuzo hiyo kutokana na ubora ambao ameonesha msimu uliopita.

Moja kati ya washambuliaji wanaotikisa Dunia huwezi kosa jina la Harry Kane anayekipiga pale Bayern Munich ambaye mchezaji huyo ameingia kwenye Kundi la wachezaji ambao wanaweza kubadilisha historia ya klabu na Taifa.

Msimu wa 2025/26 akiwa Bayern Munich alifunga mabao 61 katika mashindano yote, akashinda Bundesliga na DFB-Pokal, huku akitwaa Golden Shoe ya Ulaya. Pia alifunga mabao 36 Bundesliga, 14 Champions League na 10 DFB-Pokal. Jisajili hapa.

Ukiachilia mbali kuwa Kane ni tunu ya Klabu na Taifa, pia ni mshambuliaji anayeweza kucheza kama namba 9 na wakati huo huo mtengeneza nafasi kwa wenzake na hii inampa mwanya wa kuwa na rekodi nzuri zaidi na kumfanya kuwa hatari zaidi akiwa karibu na lango la mpinzani.

Na jambo la kuvutia zaidi ni kwamba rekodi zake bado zinaendelea kuvunjika. Septemba 2026 alifikisha mabao 100 ya Bundesliga katika mechi 98 pekee, akiwa mchezaji aliyefikisha idadi hiyo kwa kasi zaidi katika historia ya ligi. Katika mchezo dhidi ya Union Berlin alifunga mawili na kufikisha 101.

Jinyakulie Mamilioni kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kwa Uingereza, chini ya Thomas Tuchel Kane bado ni injini ya safu ya ushambuliaji. Katika ushindi wa 7-0 dhidi ya Croatia Oktoba 3, alifunga mabao mawili na kufikisha jumla yake ya kimataifa kwenye mabao 89 katika mechi 124. Pia amekuwa akifunga katika mechi sita mfululizo za Uingereza akiwa ugenini.

Kinachofanya mjadala wa Kane kuwa mkubwa zaidi sasa ni Ballon d'Or. Baada ya msimu wake wa kihistoria Bayern, alionekana miongoni mwa vinara wa tuzo hiyo; The Guardian hata ilimweka kileleni mwa orodha yake ya Septemba. Lakini ushindani wake ni mkubwa, hasa kutoka kwa mastaa kama Kylian Mbappé na Lamine Yamal.

Moja ya sifa za Kane ni pamoja na kufunga kwa kichwa, mguu wa kushoto, mguu wa kulia, penalty, shuti la mbali, lakini pia anaweza kutengeneza nafasi. Huo mchanganyiko wa scorer + creator ndio unaomfanya awe mshambuliaji kamili. Je Kane ataweza kuchukua tuzo hiyo?. Bashiri hapa


Tembelea Website ya Nyimbo za Injili Africa. Pakua na Kusikiliza bure bila malipoBOFYA HAPA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini