Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Watoto Dokta Faustine Ndugulile akiwasili Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii wakati alipofanya ziara kwa mara ya kwanza.
Sehemu ya Watumishi wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Watoto Dokta Faustine Ndugulile akizungumza na watumishi wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii wakati alipofanya ziara kwa mara ya kwanza.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Watoto Dokta Faustine Ndugulile akikabidhiwa ua na Afisa Utumishi Bi. Daina Lumelezi wakati alipotembelea Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Watoto Dokta Faustine Ndugulile akibadilishana mawazo na viongozi wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii mara baada ya kumaliza kuzungumza na watumishi wakati alipofanya ziara kwa mara ya kwanza.
Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Bw. Marcel Katembo akizungumza wakati wa kikao baina ya Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wanawake na Watoto.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Watoto Dokta Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na watumishi wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii wakati alipofanya ziara kwa mara ya kwanza. PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO WAMJWW
…………………………………………………………………
Na WAMJWW
Naibu Waziri wa Afya Maendelo ya Jamii jinsia Wanawake na Watoto Dokta Faustine Ndugulile ameitaka Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kuratibu shughuli znazofanywa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ili yafanye kazi kulingana na uanzishwaji wa mashirika hayo.
Dokta Ndugulile aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na watumishi wa Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii alipokwenda kujitambulisha kufuatia kuteuliwa hivi karibunoi katika mabadiliko yaliyofanyika ya baraza la mawaziri.
Alisema , pamoja na idara hiyo kuwa na kanzi data kwa ajili ya mashirika yasiyo ya kiserikali nchini lakini kuna haja ya kufuatilia utendaji kazi wa mashirika yasiyo ya kiserikali kwani baadhi ya mashirika hayo yamekuwa yakienda kinyume na kazi iliyokusudiwa.
‘”kuna mashirika yasiyo ya kiserikali ya Kimataiafa na yale ya kitaifa ni vizuri yale ya kimataifa yawe na sura ya kimataifa nay ale yenye sura za kitaifa yabaki na sura hiyo kwani wakati mwingine hasa kipindi cha uchaguzi baadhi ya mashirika hayo hujishughulisha na shughuli za kisiasa na kuacha malengo ya kuanzishwa kwake’’.
Aidha, dokta Ndugulile ameenda mbali zaidi kwa kusema baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa yakijishughulisha pia na masuala yanayoenda kinyume na maadili ya Tanzania hivyo amaitaka idara hiyo ihakikishe kila shirika lisilo la kiserikali linatumia fedha inazopatiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.
Akizungumzia suala la huduma za jamii kwa wazee, Dk Ndugulile alisema, pamoja na jitihada zinazofanyika katika kuwahudumia wazee bado eneo hilo lina changamoto kubwa hususan katika misamaha ya kuhudumia wazee katika huduma za afya pamoja na nyumba za kuwatunza wazee.
Alisema katika vituo vya kuhifadhia wazee kumekuwa na changaomoto nyingi na wakati mwingine kulazimu vituo hivyo kusaidiwa na watu wengine tofauti na idara husika katika huduma mbalimbali kama vile huduma za umeme.
Aidha, ameshauri kupitiwa upya kwa Sera, Sheria na Miongozo ya Idara kuu ya maendeleo ya jamii kwa kuwa sera Sheria na miongozi iliyopo haendanane na wakati uliopo sasa.
Amewataka watumishi wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kuwa wabunifu kwa rasilimali chache zilizopo na kufanya tafiti wakati wa kufanya kazi zao na kusisitiza kuwa asingependa watumishi watofautiane naye katika ufuatiliaje wa shughuli za Wizara.
Hivi karibuni Wizara ya Afya kupitia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii iliendesha zoezi la la kuhakiki mashirika yasiyo ya kiserikali kwa lengo la kuhuisha orodha ya mashirika hayo na kuboresha kanzi data ili kupima utekelezaji wa majukumu ya mashirika hayo.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA
0 Comments