NISHATI YA UMEME NI KIUNGO MUHIMU KUCHOCHEA UWEKEZAJI WA VIWANDA”-DKT MWINUKA

NISHATI ya  umeme imeelezwa kuwa ni kiungo muhimu katika kuchochea uwekezaji wa viwanda hapa nchini ambao utasaidia kuinua kwa kasi uchumi ikiwemo maendeleo kwa watanzania.


Hayo yalibainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) Dkt Tito
Mwinuka hivi karibuni wakati akizungumza katika baraza kuu
la 47 la wafanyakazi wa Tanesco
mjini hapa ambapo alisema kwa
kutambua umuhimu huo wataihakikishia serikali malengo yao ya
viwanda
yanatimia.



Alisema kutokana na hali hiyo wataendelea kuhakikisha umeme wa uhakika
unapatikana katika
maeneo mbalimbali hapa nchini bila kuwepo kwa
vikwazo vya namna yoyote ile ili azma hiyo
iweza kutimia kwa vitendo
na hivyo kuchochea kasi ya uchumi.


“Kama mnavyojua serikali ya awamu ya tano imeazimia kukuza uchumi nchi kufikia ule wa kati wa
viwanda hivyo kufikia azma hiyo nishati ya
umeme ni kiungo muhimu katika kuchochea uwekezaji wa viwanda ambao utasaidia harakati za maendeleo “Alisema


“Hivyo napenda kuihakikishia serikali kwamba tunatambua wajibu tulio nao katika kutimiza
malengo hayo kwa kuongeza uwajibikaji na ufanisi
kazini ambao ndio utakuwa dira ya kufikia
mafanikio “Alisema.


Kaimu Mkurugenzi huyo alisema tokea kuanzishwa kwa baraza hilo limekuwa ni sehemu muhimu
kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali kwa
maslahi ya wafanyakazi ambao wamewaamini
kuwawakilisha.


“Baraza hili limesaidia shirika kujua changamoto na kero zinazowakabili mahala pa kazi na kwa pamoja ufumbuzi wake na  changamoto hizo zimepatiwa ufumbuzi kwa faida ya wafanyakazi
na
shirika kwa ujumla “Alisema.


Alisema serikali ya awamu ya tano imeazimia kukuza uchumi nchi kufikia
ule wa kati wa viwanda
hivyo ili kufikia azma hiyo nishati ya umeme ni
kiungo muhimu katika kuchochea uwekezaji wa
viwanda ambao utasaidiam
harakati za maendeleo.

Habari kwa Hisani ya Blog ya
Kijamii ya Tanga Raha.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini