WANAFUNZI WA SHULE KONGWE NCHINI WAPANIA KUFANYA VIZURI MITIHANI YA KIDATO CHA SITA MWAKANI

mzu (1)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua miundombinu inayokarabatiwa katika shule ya sekondari Mzumbe Mkoani Morogoro.

mzu (2)

Wanafunzi na watumishi wa shule ya sekondari Mzumbe wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipofanya ziara shuleni hapo.

mzu (3)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua miundombinu katika shule ya wasichana Kilakala mkoani Morogoro.

mzu (4)

Wanafunzi wa shule ya wasichana Kilakala wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo alipofanya ziara shuleni hapo.

 

mzu (5)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikagua baadhi ya mabweni yaliyokarabatiwa katika shule ya sekondari Mzumbe.

…………..

KUNA kila dalili za kuwepo na mpambano mkali kwa shule za serikali wa kushika nafasi 10 bora hapa nchini katika matokeo ya kidato cha sita mwakani.

 

Dalili hizo zimeonekana leo katika ziara za Waziri Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo alipokuwa katika muendelezo wa  ziara yake ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa shule kongwe hapa nchini.

 

Akikagua ukarabati huo katika Shule ya sekondari ya wasichana Kilakala na Shule ya wavulana Mzumbe mkoani Morogoro, Wanafunzi wa shule hizo wamemhakikishia Waziri Jafo kuwa watahakikisha wanafanya vizuri kwenye mitihani yao kutokana na kuwepo na mazingira mazuri ya kusomea.

 

Wanafunzi na wafanyakazi wa shule hizo wametamba kufanya maajabu kwenye mitihani kwa kushika nafasi tatu bora katika matokeo ya mitihani ya kidato cha sita ya mwakani.

 

 

Katika ziara hiyo, Waziri Jafo ameonyesha kurishishwa na maendeleo ya ukarabati wa shule hizo mbili na kuhimiza ujenzi wa majengo hayo unaofanywa kwa kushirikiana na Shirika la Nyumba nchini(NHC) kukamilisha miundombinu ndani ya muda wa mkataba ambao ni tarehe 27/10/2017.

 

Hivi karibuni Waziri Jafo alitembelea Shule maalum ya wasichana ya Msalato iliyopo Manispaa ya Dodoma ambapo pia wanafunzi walimuahidi kufanya vizuri kwenye mitihani yao kutokana na mazingira ya kusomea kuboreshwa.

 

Hii ni mara ya kwanza kwa shule za serikali kuonyesha shauku ya kutaka kushika namba za juu katika matokeo ya  kidato cha sita kutokana na kuboreshwa mazingira yao ya kujifunzia.

 

Kutokana ni hali hii, ni dhahiri kuwa mwelekeo wa shule za serikali katika kipindi cha sasa na kijacho ni mzuri na shule Kongwe zitarejea kwenye ubora wake.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini