Asante Kwasi..Mchezaji pekee mwenye rekodi ya kipekee kwenye Ligi Kuu

BEKI mpya wa Simba, Asante Kwasi, ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza msimu huu kufunga magoli kwenye timu mbili tofauti kwa msimu mmoja wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Raia hiyo wa Ghana, alifunga bao moja juzi wakati Simba ilipoishindilia Singida United magoli 4-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kufikisha jumla ya magoli sita.

Hata hivyo, lilikuwa ni goli lake la kwanza kuifungia Simba kwenye Ligi Kuu tangu ajiunge na timu hiyo kipindi cha dirisha dogo la usajili akitokea Lipuli ya Iringa.

Magoli yote sita ameyafunga msimu huu wa Ligi Kuu 2017/18, matano akiyafunga akiwa na timu yake ya zamani Lipuli, hivyo kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli akiwa na timu mbili tofauti kwa msimu mmoja.

Moja kati ya magoli yake aliyoifungia Lipuli, ilikuwa ni dhidi ya timu yake mpya ya Simba kwenye Uwanja wa Uhuru, Novemba 26 mwaka jana timu hizo zilipotoka sare ya bao 1-1.

The post Asante Kwasi..Mchezaji pekee mwenye rekodi ya kipekee kwenye Ligi Kuu appeared first on Mtembezi.


Sponsored by SOMA ZAIDI

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini