BAADA YA OKWI KUFANYA MAAJABU JANA,ATOA ZAWADI YA MABAO YAKE KWA MTU HUYU,SOMA HAPO KUJUA


Baada ya kuwa kero kutokana na kuchelewa kurejea nchini, Emmanuel Okwi amejiunga na Simba na mechi ya kwanza ambayo ilionekana ngumu dhidi ya Singida United, amepiga bao mbili.

Bao hizo mbili, Okwi amezirejesha kwao Uganda kwa kumzawadia mtoto wake aliyezaliwa hivi karibuni.

Pamoja na kuwa majeruhi lakini Okwi alilazimika kubaki Uganda baada ya mkewe kujifungua mtoto wa pili.

Zawadi hiyo kwa mwanaye imetolewa mara tu baada ya mechi ya jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku Okwi akiwa shujaa wa mchezo huo katika ufungaji mabao.


Simba ilionyesha soka safi na kufanikiwa kuituliza Singida ambayo awali ilionekana ni hatari kubwa kwa Simba

Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini