BUSWITA AILIPA FADHILA YANGA KWA BAO MUHIMU DHIDI YA RUVU SHOOTING

Mabingwa wa ligi kuu Soka Tanzania bara Yanga wameibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.

Pius Buswita ambaye Usajili wake kuelekea Yanga ulizua zengwe kwani alitakiwa pia na Simba na kupelekea mgogoro mkubwa Hadi pale busara zilipotumika na kukubaliwa kucheza Yanga na ndiye aliyeipatia Yanga bao pekee Leo akifunga Kwa kichwa dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza.

Ruvu Shooting wanatakiwa wajilaumu wenyewe kwani wamekosa nafasi nyingi za kufunga katika mchezo wa Leo baada ya kukosa nafasi nyingi za wazi na kushindwa kufunga.

Kwa matokeo hayo ya Leo Yanga wanapanda mpaka nafasi ya tatu kwenye msimamo wakifikisha pointi 25 huku Ruvu Shooting wakiendelea kushika mkia wakiwa na pointi 11.

Katika matokeo mengine ya michezo ya Leo Azam FC wakiwa ugenini jijini Mbeya walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 2-0 ushindi ambao unawapeleka kileleni mwa msimamo wakifikisha pointi 30 wakiishusha Simba wenye point 29 ambao kesho watacheza na Kagera Sugar.

Ndanda FC ikisafiri mpaka Mwadui walilazimishwa sare ya bao 1-1 na wenyeji Mwadui FC katika mchezo mwingine wa ligi hiyo Leo Jumapili.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini