CHADEMA YAKUBALI KUYALAMBA MATAPISHI YAO,,YAKUBALI KUSHIRIKI UCHAGUZI UNAOSIMAMIWA NA TUME ILE ILE WALIYOIKATAA,SOMA HAPO KUJUA

WAKATI Umoja wa vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA) wakiwa wametangaza kususia chaguzi zote zitakazofanyika nchini mpaka pale Tume ya Uchaguzi nchini (NEC) itakavyotatua Dosari zilizojitokeza kwenye uchaguzi wa marudio wa kata 43,
Huku Dosari hizo zikiwa bado hazijatatuliwa hata moja ikiwemo ombi la umoja wa vya hivyo vya Chadema,Cuf,NCCR-Mageuzi,NRD la kutaka kukutana na NEC pamoja na viongozi wa Jeshi la Polisi kujadili mapungufu makubwa yalijitokeza kwenye uchaguzi huo wa marudio ambao Chama cha Mapinduzi (CCM) ilishinda kwa kuta 42 huku upinzani ikishinda kata moja.
Lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida Kamati Kuu ya Chama imemaliza Vikao vyake Leo tarehe 19 Januari, 2018 na  kuibuka  kufanya uamuzi wa kushiriki kwenye uchaguzi mdogo kwenye majimbo ya Kinondoni na Siha unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 Februari, 2018.


Baada ya uamuzi huu kufanyika , Kamati Kuu imewateua wagombea wa Majimbo hayo kama ifuatavyo;

1. Jimbo la Kinondoni ameteuliwa Mhe. Salum Mwalim Juma

2. Jimbo la Siha ameteuliwa Bwana Elvis Christopher Mosi

Wagombea wote wameshachukua fomu za uteuzi kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye majimbo husika na watazirejesha kesho Jumamosi tarehe 20 Januari 2018 , kwa ajili ya uteuzi.

Imetolewa Leo tarehe 19 Januari, 2018.

John Mrema – Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje.


Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini