MTANDAO WA KIJAMII WAJITOKEZA KATIKA KUINUA SEKTA YA UTALII NCHINI,SOMA HAPO KUJUA


Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa deiplaces Dk.Paul Bamutaze akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya kutoa taarifa sahihi za vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania.

KATIKA kuhakikisha wanainua sekta ya utalii hapa nchini pamoja na nchi jirani Mtandao wa kijamii wa kuutangaza utalii wa Deiplaces umesema umejizatiti kuiunua sekta ya utalii.
Pia Mtandao umesema pia umejipanga vema kutoa taarifa sahihi za vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania ili iweze kuwavutia watalii wengi kuja nchini.

Hayo yamesema leo na  Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Deiplaces Dk.Paul Bamutaze wakati wa mkutano na waandishi wa habari alipokuwa akiutambusha mtandao huo ambao utajikita katika kutoa taarifa ya masuala ya yanayohusu utalii.

Amesema katika mtandao huo watakuwa wakitoa taarifa mbalimbali zinazohusu utalii wa Tanzania ambapo taarifa hizo zitasomwa na watu wa mataifa mbalimbali duniani.

Amesema wanatambua juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuutangaza utalii pamoja na vivutio vilivyopo lakini nao wameona ipo haja ya kusaidia kutangaza utalii uliopo nchini Tanzania.

"Tumekuja Tanzania kwa ajili ya kuanzisha mtandao wa kijamii ambao utakuwa ukihusika na utoaji taarifa sahihi zinazohusu utalii na vivutio vilivyopo. Lengo letu ni kufanikisha kila anayetaka kufahamu kuhusu Tanzania na vivutio vyake vya utalii basi apate kutoka kwetu.

Hata hivyo Dk 
Bamutaze amesema 
mtandao huu utakuwa sehemu sahihi ya hata kwa  vyombo vya habari ambavyo vinataka kupata habari sahihi zinazohusu utalii basi watazikuta kwenye mtandao huo.

"Hakutakuwa na gharama yoyote unapotaka kupitia taarifa za utalii ambazo tunakuwa tunaziweka,"amesema. Dk.Bamutaze amefafanua unapotaka kuzungumzia Mlima wa Kilimanjaro hakuna ambaye hajui historia yake, na hivyo wao watakapoamua kutoa habari za mlima huo watajikita kuelezea maisha ya watu wanaouzunguka mlima huo pamoja na mazingira yake"amesema 

Amesema unapotaka kuizingumzia mbuga ya Serengeti ambayo ina kila aina ya vivutio vya utalii basi lazima taarifa ziwe zenye ukweli na si za kupotosha. Amefafanua wamekuwa wakitangaza utalii wa nchi mbalimbali za Afrika na sasa wanataka kujikita Tanzania.



Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini