KASEKE ATAJA SIRI ZA KIPIGO KUTOKA KWA SIMBA


Kiungo wa timu ya Singida United, Deus Kaseke amesema walifanya makosa mengi katika mchezo wa jana dhidi ya Simba na kujikutaka wakilala kwa mabao 4-0.


Nyota huyo wa zamani wa timu ya Yanga amekiri kuwa hawakuwa na siku nzuri kwani kila walichofanya hakikutimia wakati wapinzani wao wakiwa kwenye ubora mkubwa.

Kaseke amesema kilichowatokea jana sio jambo la ajabu kwani ni kawaida katika soka ambapo wataenda kufanyia kazi ili kufanya vizuri katika mechi zijazo.

"Haikuwa siku yetu kabisa, tulifanya makosa mengi na wenzetu walikuwa bora ndio maana tukapoteza kwa mabao hayo ila tunaenda kujipanga kwa ajili ya michezo ijayo," alisema Kaseke.

Singida ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo kutokana na kufanya vizuri kwenye michuano ya Mapinduzi iliyomalizika visiwani Zanzibar mapema mwezi huu wakati Simba ikienguliwa hatua ya makundi.
Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini