MFARANSA APEWA MKATABA SIMBA

Vinara wa ligi kuu Tanzania bara Simba sports Club meingia mkataba na  kocha wao  Mfaransa Pierre Lechantre ambao haukuwekwa wazi

 Lechanter ataanza kukinoa kikosi hiko baada ya kurejea kutoka Kagera, Simba iko mkoani Kagera kwa mchezo wao wa ligi kuu dhidi ya wanamkurukumbi Kagera Sugar utakaopigwa siku ya Jumatatu

Mfaransa huyo amesema anataka kuibadili Simba kuwa miongoni mwa timu bora sio tu Tanzania basi hata Afrika kwa ujumla.

"mchezo wa jana niliona timu ikifanya makosa mengi hasa kwenye nafasi ya walinzi kitu ambacho nitakifanyia kazi mara tu nitakapoanza kazi," alisema Pierre

Simba pia imeingia mkataba na kocha wa viungo Aimen Habibi raia wa Tunisia.



Sponsored by ZAMOTO MEDIA

Post a Comment

0 Comments

close
Banner iklan disini